Nehemia Kilave
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 1,414
- 3,118
Hayati Magufuli binafsi sina shaka na nia yake njema kwenye hili taifa na alionesha nia hiyo kwa mambo mazuri aliyofanya ndani ya muda mfupi .
Changamoto ni ile ile ya viongozi wa Afrika kuamini mawazo yao ni sahihi muda wote hivyo akaleta wabunge ambao hawatakuwa wanakwenda kinyume na anavyoamini ili mambo yaenda haraka akasahau kwamba kuna kifo .
Kwake yeye alikuwa na nia nzuri Changamoto ni kama ilivyotokea kaondoka kawaacha wabunge ambao ni wachache sana wenye sifa za kuwepo pale na wanafanya kile kile ambacho Hayati Magufuli alihitaji pasipo jali utashi wa yule aliye kileta kikubwa kiwe cha Serikali
Kwa hapa alitukosea sana na sawa katiba iliyopo inatoa mamlaka kubwa kwa Rais hivyo inafanya kila Rais aifurahie huku wananchi mkitegemea hekima na busara zake .
Kwa bunge hili na Katiba hii watanzania tumekosewa sana .
Nadhani ushauri kwa watanzania mnapenda kuwa viongozi siku mfikirie siku moja kutakuwa na kiongozi mwingine ambae atatumia maamuzi mliyo fanya au sheria mlizo ziweka .