Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Watanzania wenzangu hebu tutafakari hili pamoja. Hoja yangu ni kuwa bunge letu kama chombo kilichoainishwa katika katiba yetu kama muhimili wa wananchi wenye dhamana ya kusimamia na kuishauri serikali kwa niaba ya wananchi. nasikitika kusema muhimili huu umeporwa na vyama vya siasa na kuufanya uwanja wao wa kuendeshea propaganda za kuimarisha vyama vyao.

bunge ni chombo ambacho tunakitegemea kiwe na umoja katika kusimamia serikali kwa maana tunategemea bungeni tuone pande mbili tu. yaani bunge upande mmoja wakiwa kama bodi ya kusimamia kampuni na serikali upande wa pili ikija na hoja za mikakati inayotaka kutekeleza.

kitendo cha kugawa bunge letu ki vyama linadhoofisha bunge na kulipotosha bunge kwani hoja za vyama ndio zinapewa kipaumbele. hoja inaungwa mkono au kupingwa kutokana na imetolewa na upande gani? sasa kwa staili hii kweli kwa nini tusiseme kuwa utaratibu tuliojiwekea unalipotosha bunge letu.

Hivi kweli ukiwa na bodi ya kusimamia kampuni iliyogawanyika inaweza kuwa na ufanisi kweli? Ni madhambi mangapi ambayo bunge linayanyamazia kisa bunge limegawanyika ki vyama, ni mara ngapi tumeona kambi moja ikiweka msimamo maovu fulani yakemewe lakini kambi ya walio wengi ikipuuza, rasimali za taifa zinaporwa na wizi huo ukihalalishwa? ni wakati wa kutafakari ni wapi tulipokosea.

Suluhisho hapa ni kurejesha utawala kwa wananchi, na wananchi kwa umoja wao mhimili wao ni bunge hivyo ili kurejesha utwala kwa wananchi ni kurudisha bunge kuwa mhimili wa wananchi kutoka kwa vyama vya siasa vilivyopora mhimili huu. hii itafanyika kwa kila mbunge anayeingia bungeni kwa tiketi ya chama, anapoingia bungeni chama chake kinabaki mlangoni, mbunge awe ni mwakilishi mkazi wa eneo husika mda wote akifanya kazi katika ofisi ya mbunge jimboni kwake, kazi yake ni kufuatilia miradi ya maendeleo iliyopitishwa utekelezaji wake, kusikiliza matatizo ya wananchi na bungeni anakuja akiwa na takwimu alizokusanya jimboni kwake na huo ndio mjadala wa bunge.

mbunge awe full time mbunge na hapa tutakuwa tumetenga siasa na biashara kwa kiwango fulani. tunataka bunge liwe kitu kimoja katika kutetea wananchi. mojadala ya vyama irudi TCD
 
mbona mnasoma kimya kimya hata hamtoi maoni?
 
bunge tumeliweka kwa umoja wao kusimamia serikali kwa niaba yetu wananchi
 
likasimamie utendaji wa serikali sio huyu anasema huyu awajibishwe huyu anapinga ingawa ndio demokrasia lakini kumbuka nyumba yako ukiweka demokrasia mtoto anatenda kosa mnaanza baba anasapoti mama anapinga ndio mwanzo wa kuaribikiwa mtoto.

tunataka sauti moja kusimamia mapato na matumizi ya serikali, tunataka sauti moja katika kusimamia utendaji wa serikali, tunataka sauti moja katika kusikiliza matatizo ya wananchi na kuwasemea
 
Hii ni sahihi kabisa labda kuweka hili vizuri zaidi ni kwamba wabunge hasa wa ccm wanawakilisha chama na sio wananchi. Nadhani katiba mpya inabidi tuwe na kipengele/provision ya kumwondoa mbunge madarakani wakati wowote wapiga kura wanapohisi kuwa kinachowakilishwa ni chama na sio wao na mfano mzuri ni hoja inayoendelea bungeni leo ya wizara ya mifugo ambapo ni dhahiri shairi kwamba imetengewa budget ndogo sana na hadi sasa wabunge wengi wameikataa ila kuna wasaliti wachache (waccm) wameunga mkono kwa maana ya kuisaidia serikali na sio wapiga kura wao ambao wengi wao ni wafugani sasa hawa niwakuwaondoa.
 
Sijaona bunge bado! TZ hatuna bunge tuna uwanja wa mipasho tu. Watu wazima kunyoosheana vidole kama wako ngomani ndio nn ss??

Sijawahi ona wabunge wanasutana popote duniani ila TZ
 
Back
Top Bottom