Bunge la Katiba halina mamlaka kisheria kubadili chochote kilicho ndani ya rasimu!

Bunge la Katiba halina mamlaka kisheria kubadili chochote kilicho ndani ya rasimu!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Ukirejea katika sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyoridhiwa na Bunge la Jamhiri ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kuwa SHERIA rasmi,utaona yafuatayo:

1. Tafsiri ya kifungu cha 25 (2)cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba juu ya Majukumu ya Bunge la Katiba Mpya inasema hivi: "Bunge Maalumu la Katiba litakuwa na jukumu la kuijadili rasimu ya Katiba na kuipitisha tu"

Sheria hii ya mabadiliko ya Katiba inalifunga Bunge Maalumu la Katiba kuishia katika kujadili na kupitisha rasimu hiyo bila kuondoa neno wala kuongeza neno litakalobadili maana ya neo hilo.

Vivyo hivyo Bunge la katiba litafanya kazi ya kuboresha masharti ya Katiba yaliyomo ndani ya rasimu ya Katiba pasipo kuweka masharti mapya ambayo kwa taathira yatabadili ama kufifisha masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Rasimu hii ya Katiba Mpya.

Kwamaana nyingine nikuwa chombo pekee cha kubadili vifungu vya rasimu ile ya mzee wetu Warioba ni Bunge la Jamhuri na sio hili Bunge la Katiba,

Sasa msimamo wa ccm kuwa wao wanataka serikali mbili unatoka wapi ilihali katika rasimu hakuna pendekezo la serikali mbili wala moja, bali ni serikali tatu tu iliyopendekezwa na Watanzania 64%?

Taarifa zinasema ccm imechomeka rasimu mbadala huko Bungeni na kutia hofu kuwa huenda rasimu ya Watanzania iliyoratibiwa na Mzee wetu Warioba imetiwa kapuni.
 
kumbe wamechomekea kimeo chao badala ya ile ambayo watanzania asilimia 64 walioamua !
 
Dawa iliyopo kwa hawa magamba ni kwenda mahakamani ili kusimamisha mchakato mzima wa katiba kwani huu ni usanii mtupu.Bora hizo ela wangenunulia madawati
 
Sasa ya nini kujadili kama hakuna room ya mabadiliko?

walichoruhusiwa ni kusema ' HOW ' na wala siyo kusema ' WHY ' au ' NO ' wala hawaruhusiwi kuchomeka vitakataka vya SERIKALI 2 , 5 AU 7 , maana asilimia 64 wamesema 3 , je umeelewa ?
 
Dawa iliyopo kwa hawa magamba ni kwenda mahakamani ili kusimamisha mchakato mzima wa katiba kwani huu ni usanii mtupu.Bora hizo ela wangenunulia madawati

wala usihofu , hakuna DIKTETA yeyote aliyewahi kuushinda UMMA .
 
Ndio maana wameamua nakuiingiza sheria ya kutokuhusiha kamati kuu ya jaji warioba kutowhiriki kwenye bunge la katiba ili wafanye hayo madudu yao....ccm bhana!!!!!!!!
 
Ndio maana wameamua nakuiingiza sheria ya kutokuhusiha kamati kuu ya jaji warioba kutowhiriki kwenye bunge la katiba ili wafanye hayo madudu yao....ccm bhana!!!!!!!!

Watafaya hivyo lakini bado sheria inasimama palepale, jambo mhimu ni kushinikiza wafute sheria na waheshimu
 
Mimi nasuburi niujue mwisho wa haya yote, maana posho inajadiliwa siku nzima, sijui katiba itachukua muda gani aisee
 
Hapa ni kupoteza pesa za walipa kodi masikini wa nchi hii, hakuna dalili ya uwezekano wa kuafikiana na kupata katiba mpya, kila upande unajali maslahi ya kichama tu na wasio na chama wanalilia nyongeza za posho, just wasting of time n money mwhisho wa siku ni katiba ileile ya 77.
 
Wameshindwa kukaa nakujadili kanuni eti wanalilia posho.
 
Ina maana kukaa kwao dodoma miez mitatu ni bure? hata mh. rais alishasema msimamo wa chama chao juu ya hilia. mabadiliko yatakuepo tuu.
 
Back
Top Bottom