Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Mwalimu Nyerere Ideology Conservatiom Society ya jijiniTanga,imefungua kesi mahakama kuu kupinga mchakato wa katiba mpya unaoendelea mijini Dodoma kwa sasa
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Dr.Kalokola amesema sababu za kupinga mchakato huo ni wananchi kukosa wawakilishi waliowachagua kwa ridhaa yao,posho kubwa wanayolipwa wajumbe na gharama kubwa za kuandaa Bunge hilo.
Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa wajumbe wote ikiwa ni pamoja na wale wa kutoka katika taasisi mbalimbali hawakuchaguliwa na wananchi kuwawakilisha na hivyo wao pamoja na wabunge hawana ridhaa ya wananchi.
Kuhusu posho kubwa,mkurugenzi huyo amesema serikali inashindwa kuwalipa watumishi wake stahiki zao kama vile walimu huku ikiwalipa wajumbe hao posho hiyo ya sh 300,000 kwa siku.
Kesi hiyo ilifunguliwa February 17 mwaka huu sasa inasubiri kupangiwa jaji wa kuisikiliza.
Kwa taarifa zaidi,visit :Mwananchi: mwanzo - Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
CHANZO:Mwananchi
MY TAKE:
Wana hoja za msingi .