Bunge la Katiba lapingwa mahakama kuu

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Mwalimu Nyerere Ideology Conservatiom Society ya jijiniTanga,imefungua kesi mahakama kuu kupinga mchakato wa katiba mpya unaoendelea mijini Dodoma kwa sasa

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Dr.Kalokola amesema sababu za kupinga mchakato huo ni wananchi kukosa wawakilishi waliowachagua kwa ridhaa yao,posho kubwa wanayolipwa wajumbe na gharama kubwa za kuandaa Bunge hilo.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa wajumbe wote ikiwa ni pamoja na wale wa kutoka katika taasisi mbalimbali hawakuchaguliwa na wananchi kuwawakilisha na hivyo wao pamoja na wabunge hawana ridhaa ya wananchi.

Kuhusu posho kubwa,mkurugenzi huyo amesema serikali inashindwa kuwalipa watumishi wake stahiki zao kama vile walimu huku ikiwalipa wajumbe hao posho hiyo ya sh 300,000 kwa siku.

Kesi hiyo ilifunguliwa February 17 mwaka huu sasa inasubiri kupangiwa jaji wa kuisikiliza.

Kwa taarifa zaidi,visit :Mwananchi: mwanzo - Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza

CHANZO:Mwananchi

MY TAKE:
Wana hoja za msingi .
 
Swali langu ni kuwa,hii kesi ikishaanza kusikilizwa,mchakato huu utaendelea?

Wanasheria mtusaidie.
 
Hiyo taasisi iko sawa kwan haiingii akirin wajumbe hao wa Bunge maalumu kdai posho ya Tsh 300000/day haitoshi wakat mie raia wa kawaida hapa dodoma hyo ndo pato langu kwa mwaka.Anaeona posho haitoshi aende akafanye kaz inayompatia pesa nyng zaidi.
 
Sizani kama mchakato wa katiba utasitishwa kwa kesi hii. Japo wana hoja ya msingi kwa kweli ila wamechelewa mno.
 
Hiyo taasisi nimeikubari maana ni kweli kabisa hakuna mwanaichi aliyewapa ridhaa ya kwenda dodoma nakuijadili rasimuya katiba mpya afu nashangaa kabisa eti mjumbe anasema nimetumwa na mwanainchi niitee hii rasimu.
 
Naona kama huyu Dr anatafuta umaarufu kwa kuandikwa kwenye vyombo vya habari!
 
Naona kama huyu Dr anatafuta umaarufu kwa kuandikwa kwenye vyombo vya habari!

Huo umaarufu ni matokeo tu cha msingi angalia ni nini anafanya kwa nchi yake.

Mbona hata Hitler alikuwa maarufu kwa ukatili wake?!
 
Sizani kama mchakato wa katiba utasitishwa kwa kesi hii. Japo wana hoja ya msingi kwa kweli ila wamechelewa mno.
Hivi swala la kuchelewa linaweza kuwa hoja mahakamini?
 
Mchakato wa kuandika katiba haukuridhiwa na Bunge?Mhimili miongoni mwa mihimili isiyoingiliana?
Unapokuwa na phd holder asiye makini n majanga.
Ulianza kama muswada then ukawa sheria ya mabadilko ya katiba kwa kutiwa saini na mwenye mamlaka. "Rais" kwa niaba ya wa Tz.
 
afadhali hao kuliko wanaharakati wanaopiga kelele bika kuchukua jukumu lolote ukweli wajumbe wa bunge la katiba hawawezi kudai wanawakilisha wananchi wakati hawana ridhaa ya wananchi,pia bunge limejaa wanasiasa kama vile katiba yetu itakuwa inazungumzia mambo ya siasa tu,haijulikani ni vigezo gani wametumia kujilipa posho ya shilingi 300,000/= wakati hali halisi inaonyesha hatutapata katiba inayowakilisha mawazo ya wananchi,wengi wameingia kutetea misimamo ya vyama vyao
 
Hizo hoja zote zilishajibiwa bungeni kwa wale waliokuwa wanafuatilia bunge through tv kama kina sisi.
Labda wanatafuta umaarufu
 
wakili msomi msando, hebu tuwekee pingazimizi la kuendelea kwa mchakato huu wa katiba.
 
Hizo hoja zote zilishajibiwa bungeni kwa wale waliokuwa wanafuatilia bunge through tv kama kina sisi.
Labda wanatafuta umaarufu

Mahakama ndio chombo pekee cha kutafsiri sheria na sio Bunge.
 
Huo umaarufu ni matokeo tu cha msingi angalia ni nini anafanya kwa nchi yake.

Mbona hata Hitler alikuwa maarufu kwa ukatili wake?!
Salary Slip, wewe kwa mawazo yako unaamini kabisa huyo Dr atakwenda mahakani na kutakuwa na kesi? Hivi alikuwa nchi gani mpaka mchakato umefika hapa uliopo!
 
Salary Slip, wewe kwa mawazo yako unaamini kabisa huyo Dr atakwenda mahakani na kutakuwa na kesi? Hivi alikuwa nchi gani mpaka mchakato umefika hapa uliopo!

Mkuu,kwa mujibu wa gazeti,kesi imeshafunguliwa na kinachosubiriwa ni kupangiwa jaji wa kuisikiliza tu.

Labda serikali ifanye uhuni kwa kuingilia hii kesi ila hawa jamaa wakijipanga vizuri wanaweza kushinda na tukabaki midomo wazi.

Hivi nikuulize,hawa wabunge wanaweza kweli kupitisha kifungu cha kuweka ukomo kwa wabunge?

Je,wabunge wengi wa CCM wanaweza kukubali serikali 3?

Wabunge hawa wako tayari kuona baadhi ya majimbo ya uchaguzi yakifutwa kwasababu ya muundo wa serikali 3?

Wabunge wa CCM watakubali Raisi ashitakiwe?

Wabunge hawa watakubali mawaziri wasitokane na wabunge?

Hiyo ni mifano michache tu ambayo inatia shaka kama kweli wabunge hawa watatenda haki.
 
Bunge hili hawakai kivyama. wala hakuna party kokasi.
Hakuna mbunge wa ccm wala cuf. Wote ni Wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba. Tusipotoshane.
 
Ninakuhakikishia hakuna kesi hapo. Tusubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…