Bunge la katiba linajadili yaliyomo tu! Kwenye rasimu au?

Bunge la katiba linajadili yaliyomo tu! Kwenye rasimu au?

obama sererea

Senior Member
Joined
Mar 13, 2012
Posts
101
Reaction score
37
wanavyojua mimi bunge la katiba litakwenda kujadili yaliyo ndani ya rasimu tu! Na sio yasiyokuwemo. Swali langu hapa ndugu zangu ni sehemu gani ndani ya rasimu ya imeandikwa serikali mbili?
 
waliohojiwa na tume wengi waitaka serikali 3 ila kwa sasa wengi wetu tunataka serikali 1
 
Unajua kuna tatizo la uelewa na tatizo la ushabiki.
Kwa mawazo yangu ninaona kabisa wengi wanakwenda kusimamia maslahi ya vyama vyao badala ya kwenda kusimamia maslahi ya taifa lao. Na hili tatizo nafikiri linatokana na aina ya wajumbe tulionao.
 
Kiukweli kabisa sizani kama hao wajumbe walipata (1) muda wa kusoma rasimu na maudhui yake (2)sizani kama waliandaliwa kisaikologia kubeba mustakabali wa taifa, maana itakuwa haina maana wabunge kwenda kufuta mawazo ya wananchi wanaowawakilisha.
 
Inasikitisha sana pale ambapo majority wanaonekana hawajawa tayari kisaikolojia
 
wanavyojua mimi bunge la katiba litakwenda kujadili yaliyo ndani ya rasimu tu! Na sio yasiyokuwemo. Swali langu hapa ndugu zangu ni sehemu gani ndani ya rasimu ya imeandikwa serikali mbili?
rasimu itatumika kama muongozo tu wa majadiliano ya bungo,ingawa bunge litakuwa na mamlaka hata ya kuibadili rasimu nzima na kuandika katiba nyingine kabisa mfano wakaamua muundo wa muungano uwe serikali moja tu!
 
Back
Top Bottom