Bunge La Katiba Lisiporushwa Live Wanaoipenda Tanzania Bila Kujali Itikadi Tokeni Nje

Bunge La Katiba Lisiporushwa Live Wanaoipenda Tanzania Bila Kujali Itikadi Tokeni Nje

Kuntakint

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,767
Reaction score
1,526
Itakuwa si haki kwa serikali na TBC yetu, mali yetu tunayoilipia kodi kutokurusha bunge letu la kutunga katiba yetu (Wananchi). Katiba ni mali yetu si mali ya Serikali, CCM, CHADEMA, CUF, NCCR na vyama vingine.

Tunayo haki ya kusikiliza live kinachozungumzwa na kuona kama kweli wawakilishi wetu wanavyotuwakilisha, ili tujue wale wanaotetea yale ambayo tumewatuma.

Hapa inavyoonekana Serikali inataka kufichaficha ili itakapoibuka unaambiwa Serikali mbili imepita tuipigie kura, pasipo sisi wenye katiba bila kusikiliza au kuona kinachoendelea.

Wapenda nchi yao (Tanzania) wasio na vyama na wenye vyama tunawaomba kama kweli Serikali itazuia kurusha matangazo live tunawaomba msiendelee na bunge.

Waachieni hao CCM na wanaotaka katiba bila kutushirikisha sisi wenye katiba (Wananchi) waendelee na tutapambana nao kwenye kura ya kuipitisha na watakapokuja kwenye uchaguzi kuanzia mwaka huu na mwaka ujao.

Mfano mdogo tu jana kutotuhusiwa waandishi wa habari kuingia bungeni imesababisha/tumepata usumbufu wa kutopata habari za uhakika kutoka bungeni. Haki yetu (Wananchi) kuona/kusikiliza live toka tarehe 18/02/2014 hadi mwisho wa bunge, tunahaki ya kuona kila kitu kinachoendelea hata kama kuelekezana kanuni.
 
Kweli mkuu katiba ni jambo la kitaifa na jambo la kushangaza ni kwamba hata TBC ambayo ni kodi ya wananchi wanasuasua sana
 
Hii Katiba ni ya ccm wala sio ya Taifa.!
 
ni ajabu lakini kweli ndo tumeanza kwa hivo; haifai hata kidogo kwa bunge kubwa kama hili la kihistoria kwenda kimya kimya
 
Una hoja nzuri ila sasa hao Watanzania unawaambia jambo hili wala hataona umuhimu wake, ni wachache tu wanaoelewa nini maana ya kuwa na uwazi katika mchakato mzima. Nina wasiwasi kwa kuwa wajumbe wengi hata wale wa asasi za kiraia na makundi maalumu wana itikadi za CCM. Kwa hiyo tujiandae kuona hoja zinazoungwa na CCM kupita kwa nguvu kubwa sana.
 
Back
Top Bottom