Bunge la katiba liwe na lengo la kufikiwa kila siku (milestone)

Bunge la katiba liwe na lengo la kufikiwa kila siku (milestone)

East African Eagle

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
3,759
Reaction score
2,206
Bunge la katiba liwe na lengo (milestone) ya kufikiwa kila siku.Waweke utaratibu kuwa kwa siku wajadili nini na lazima wamalize hata kama mjadala huo utakamiliki saa kumi alfajiri lazima ukamilike hakuna kulala.Hii spidi wanayoenda nayo inatukera.Wengine uvumilivu na uzalendo utatuishia.

Waweke milestone na waambiane kabisa leo tutajadili kanuni mfano 10 na hatutoki hadi tumalize.Bila kuwa na milestone hili bunge litaisha 2030.Wajifunze kuweka milestone na iwe marufuku mtu kurudia rudia hoja iliyosemwa na mwingine.Spika awakalishe chini watu wasio na hoja wale akina naunga mkono alichosema mwenzangu.
 
Aaaahhh wapi posho je!! Taratibu wewe wengine humu tupo kisa posho! Mods be fair toeni hii thread!
 
Kweli aisee! Na wale wa kutoa shukrani nao pia waache.
 
Kweli aisee! Na wale wa kutoa shukrani nao pia waache.

Yaani kweli waache kupoteza muda kutoa shukrani.Unakuta mtu anaanza kumshukuru mungu,kisha kushukuru raisi aliyemteua,kisha anashukuru spika na kisha anshukuru familia yake mama watoto wake,mume wake na wanae na halafu anashukuru na kupongeza wajumbe walioteuliwa na wananchi wanaomsikiliza na waandishi wa habari waliomo bungeni n.k hapo bado hoja yake bado hajaanza inakera na kupoteza muda.

Wajumbe waende kwenye hoja moja kwa moja.Na wasirudie hoja ya mwengine.Mfano mtu kasema kura iwe ya siri hiyo hoja iandikwe ihesabiwe tayari imeshasemwa asisimame mwingine kuirudia.Spika aulize kama kuna mwingine mwenye hoja tofauti na hiyo akisimama anayesema kura iwe ya wazi basi spika achukue hiyo hoja.Aulize kama yuko mwingine mwenye hoja tofauti na hizo mbili ndiye ampe nafasi.Lakini kuendekeza tu wa akina naunga mkono aliyesema kura ya wazi na naunga mkono aliyesema kura ya siri ni mjadala usio na maana.Wajumbe wanamaliza siku wakiwa wamechoka bure tu.Kama kukionekana hakuna hoja ingine mpya uamuzi ufanyike iwe kwa kura au vyovyote hoja zingine ziendelee.Mjadala wowote sio kurudia rudia hoja iliyokwisha semwa.Spika awe mkali kukalisha chini warudia hoja na watoa shukrani ndefu kabla ya hoja na baada ya hoja.

Na ile wale wajumbe wafanya fujo za kuzomea na wanaosimama bila kuambiwa simama uongee dawa yao kuwatoa nje na kuwanyima posho ya siku hiyo.Wakinyimwa posho nina hakika wakirudi kikaoni watatulia vizuri mno.
 
Back
Top Bottom