BUNGE LA KATIBA: Taratibu zake zitakuwa vip? Spika/N.Spika ni wale wale?? Vp Majibu ya NDIYOOOOO..?

BUNGE LA KATIBA: Taratibu zake zitakuwa vip? Spika/N.Spika ni wale wale?? Vp Majibu ya NDIYOOOOO..?

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
Kwa wale wajuzi na wenye uelewa mpana wa jambo hili la Bunge la Katiba,
taratibu zake zitakuwa ni sawa na zile za Bunge la kawaida ama zitakuwa vip??

Viongozi wake watakuwa kina nani mfano Spika/N.Spika?? Ninafahamu ya kuwa
Wabunge wasasa hiviwatakuwepo ndani ya hilo Bunge,,,Je wataingia na nyadhifa zao???

Kwa wale Wabunge wapenda VURUGU, MATUSI na KUPIGANA vipi watapata nafasi ya
kuonyesha "VIPAJI" vyao???
Swali la mwisho; Bunge lina taratibu zake na kanuni za kuliongoza...Hapa katika Bunge la
Katiba ni kanuni zipi zitakazo tumika kuliendesha???

Hongereni kwa mlio chaguliwa, hela iko ya kutosha lakini pia ni nafasi yenu pia kujitangaza
upya kwa wananchi.

Mandla.

warioba+px.jpg
 
Hongereni kwa mlio chaguliwa, hela iko ya kutosha lakini pia ni nafasi yenu pia kujitangaza
upya kwa wananchi.

Mandla.
Imeandikwa - mwenye nacho huongezewa!! laki saba per day uchangie hoja usichangie zimeingia - Mungu akupe nini ndugu yangu!!

Hayo ya hela si muhimu sana, hoja ya msingi watupatie katiba ambayo itakuwa mtetezi wa wanyonge hasa wakulima na wafugaji ambao ndiyo sekta inayoajiri watu wengi takribani 80% ya wananchi wa Tanganyika.

Pia watuache kila mmoja aongoze mji wake mwenyewe kutokana na mila na desturi zake, kwa maana M -Tanganyika aangalie Tanganyika yake na M- Zazibar naye ajiangalie mwenyewe, mambo ya kuungana yawepo ambayo hayatatuletea manunguniko rohoni kwetu kila siku. Hawa wameshakuwa ndugu zetu wala hatutatengana kabisa kwa kuuhuisha utanganyika wetu na uzanzibar wao kama ilivyokuwa kabla ya mwaka 64.
 
Ombi langu maalum Job Ndugayi asiwe mwenyekiti wala spika asije fukuza wajumbe wanaochangia sana nje sababu tu eti wamechangia toka asubuhi,ref.Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom