Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Ushauri wangu kwa Bunge la Katiba ni kuwa mambo ya serikali 1,2,3,4 yasubiri hadi baada ya katiba mpya kupatikana. Hii ni kwa sababu zifuatazo:
1. Kwenye hadidu rejea kwa Tume ya Waryoba suala hilo halikuwamo.Tume haikuwa na madaraka ya kuyaingiza humo kwa kisingizio cho chote na kwa kweli ni utovu wa nidhamu kwa aliyewapa hizo hadidu rejea ambaye ndiye
aliyewateua. Tume ilihoji chini ya asilimia 1% tu ya Watanzania hivyo kisingizio kuwa hayo ni maoni ya Watanzania
wengi haina mantiki. Halafu kwa mfano kama walio wengi wa wahojiwa wangesema hawataki Muungano hiyoTume
ingekuja na rasimu ya katiba ya serikali gani? ya Tanganyika?. Pia tukumbuke kuwa hasa kwa masuala ya msingi
si lazima maoni ya wengi yashinde; tukumbuke kwa mfano katika kura za maoni za kurejesha mfumo wa vyama
vingi kura za minority ndizo zilishinda na matunda yake tunayafurahia.
2. Jamani tusidanganyike. Muungano wa serikali 2 umedumu miaka 50, tukiwa na amani na pamoja. Tumeuzoea na
hauwezi kuondolewa kirahisi rahisi hivyo na nchi inaweza kuyumba. Hebu fikiria kwa mfano (na hii inaweza kabisa
kutokea) matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 yakawa hivi:
- Rais wa Muungano .......... Mgombea binafsi Mzee EL
- Rais wa Tanganyika ........ Mgombea wa CCM Mh X
- Rais wa Zanzibar ......... Mgombea wa CUF Mzee Seif
Sasa niambie kama hapo patatosha kweli? Eti Tanganyika ndiye atakuwa mchangiaji mkuu wa fedha kwa huyo wa
Muungano? Kweli hapo kutakuwa na utulivu huko Unguja na Pemba? Jee Muungano ukivunjika hayo majeshi na
dhana zake tutayagawana kivipi?
3. Jamani tutengeneze tu kwanza Katiba Mpya, ndani ya Katiba hiyo tuweke tu vipengele vya taratibu zitakazobidi
kufuatwa za namna ya kubadili aina ya Muungano au kuvunja Muungano pale upande mmoja utakapona inafaa.
Hakuna Muungano wa aina yo yote ile ambao hauna changamoto au kero. Wakati mwingine changamoto/kero
ndiyo raha za kuungana: ni kama kwenye ndoa, suluhu yake siyo kuongeza mke au mume au kutoa talaka -
kufanya hivyo ni kuongeza matatizo.
Mchakato wa aina ya Muungano tunaotaka utakuja pale mmoja wapo wa pande zilizoungana atakapoamua kuleta
hoja hiyo kwa utaratibu utakaowekwa kwenye katiba hii mpya na siyo kwa utaratibu huu wa kudandia wa Tume
ya Waryoba. Si tume ya Waryoba, Nyalali, G55 n.k. bali ni upande moja wapo wa Muungano ndiye mwenye
mamlaka ya kuanzisha mchakato huo kwa utaratibu wa Katiba tunayotunga sasa. Ndiyo maana hadidu rejea kwa
Tume ya Waryoba hazikuwapa mamlaka hayo.
4. Ushauri wangu ni kuwa Bunge la Katiba lisijadili sana hoja ya serikali 2 au 3 maana kufanya hivyo tunaweza
kukosa katiba mpya. Baadhi ya Watanzania walishauri tangia mwanzo kwamba wanasiasa wasihusike katika
mchakato mzima wa Katiba mpya. Hili lilishindikana, kwa hiyo mchakato huu ni wa kisiasa na kwenye siasa
CCM ndiyo vinara kwa sasa tupende tusipende. Hivyo sera ya serikali 2 aidha itapita (ikipita tunapata katiba
mpya) au itakuwa draw match (hapo hatutakuwa na katiba). Hayo yalikuwa ni maneno ya Rais wa JMT
ambayo hayapaswi kupuuzwa. Sera ya serikali ya Tanganyika muasisi wake ni Mch Mtikila ambaye kwa bahati
nzuri na yeye ni mjumbe wa Bunge hilo la Katiba hivyo mjadala utakuwa moto kweli kweli lakini CCM ndiye
mwenye uamuzi.
5. Tume ya Waryoba na hata hili Bunge la Katiba haina 'mandate' ya Watanganyika kutunga Katiba ya Tanganyika.
Mchakato wa kutunga Katiba ya Tanganyika kama suala la serikali tatu litapita hauwezi kufanywa ki urahisi
rahisi kwa ku copy & paste mawazo ya Tume ya Waryoba.
6. Undugu/Muungano wa Bara na Zanzibara ni wa tangu hata wakoloni na waarabu kufika maeneo haya.
Haukuanza 1964. Bila muungano huu usalama wa pande zote mbili utakuwa wa mashaka: 'this is a geographic
fact which we cannot change". Mambo ya serikali tatu yangekuwa na mshiko zaidi kama tungekuwa tumeungana
na li nchi kubwa kama DRC. Haya Mwalimu Nyerere aliyaona mapema.
7. Ninaomba wana JF tuendelee kuwapa maoni na ushauri wabunge wa Bunge maalum la Katiba katika vipengele
mbali mbali za rasimu ya katiba watakazokuwa wakizijadili kwa siku 90 zijazo. Ninatumaini wengi wao watakuwa
wanazisoma. Ninawaomba Mods wangeweka kwenye sticky ushauri/maoni ya hoja kwa Bunge la Katiba. Ushauri
ujikite kwenye hoja na siyo kwenye ushabiki wa kisiasa. Hii itatoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi kushiriki
katika utungaji wa katiba yao kwa njia ya ki electronic.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.