EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,100
Tangu Bunge la awamu hii lianze, kumekuwa na wingu kubwa la upuuzi unaondelea kiasi cha kuanza kutia kichefuchefu. Siku hizi ni rahisi sana kubashiri nini kitatokea leo bungeni na si kama ilivyokuwa zamani. Ningefurahi sana kama madabiliko haya yangekuwa chanya kuelekea kwenye ubora lakini nachelea kusema kwamba badala yake limekuwa bunge la upuuzi, ujinga na utoto.
Kinachonikera zaidi ni kuona namna wabunge badala ya kujadili mambo muhimu juu ya mustakabali wa nchi yetu, bungeni sasa kumejaa utumbo, maneno ya mtaani, matusi, methali za khanga na ubabe wa kipuuzi kiasi cha kunifanya nijiulize kama kodi yangu ndio inawalipa wale watu pale ndani kufanya upuuzi ule wa kipuuzi. Ni kawaida sasa kuona hoja nyingi tena nyingine zenye maana kubwa kwa nchi yetu zikipingwa kwa itikadi ya vyama kwasababu tu zimetolewa na mtu kutoka upande mwingine (what the hell is this!!?)
Jamani lazima wabunge wetu mjue kwamba wananchi wa sasa sio wale wa mwaka ule, hawa wa sasa wanajua kuchuja na kupembua (tumejionea wenyewe kule Mtwara na Lindi) hebu tuweni serious la sivyo ipo siku wananchi hawa watawadai kodi zao zote mlizowahi kula kwa kwenda kufanya upuuzi ule mnaoufanya kule Bungeni.
"Bunge la kipuuzi hufanya mambo ya kipuuzi na watu wapuuzi"