Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Baada ya kikao kilichochukua muda mrefu, hatimaye Bunge la Congress limemthibitisha Joe Biden kuwa Rais wa Marekani na Kamala Harris kuwa Makamu wa Rais kwa muhula unaotarajiwa kuanza rasmi Januari 20, 2021 kwa kura 306 dhidi ya Donald Trump aliyepata kura 232.
Hatua hii inaashiria kukamilika rasmi kwa uchaguzi wa Marekani na kuwahakikishia Biden na Harris kuapishwa hapo Januari 20, licha ya jitihada za Trump kuzuia kufanikiwa kwa tukio hilo.
Trump akubaliana na uamuzi wa bunge
Rais anayemaliza muda wake, Donald Trump ametoa kauli kuwa anakubaliana na uamuzi wa bunge licha ya kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi huo, akiahidi kuwa kutakuwa na makabidhiano ya madaraka kwa njia ya amani hapo Januari 20.
Chanzo: Al Jazeera