Bunge la Tanzania balaa, kuna wakati hushambuliana kwa misingi ya kikabila na kiasili, mara rudi kwenu Oman, rudi kwenu Congo

Bunge la Tanzania balaa, kuna wakati hushambuliana kwa misingi ya kikabila na kiasili, mara rudi kwenu Oman, rudi kwenu Congo

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Wenzetu hawa wanavyopenda kuchachamaa kuhusu ukabila kwetu utadhani kwao ni binguni hamna aina yoyote ya ubaguzi, ilhali mitandao ya kijamii huanika uozo wao haswa kwenye bunge ambapo mizuka ya wabunge husababisha wanaanza kushambuliana kwa misingi ya kikabila, kikanda na asili ya mtu, mara rudi kwenu Yemen, mara huyo ni Mkongoman arudi kwao Congo.

Mitandao ya kijamii imesababisha wanafiki wengi dunia hii kuanikwa mchana peupe, unachobwatuka kinasambazwa dunia yote wanakuona, uchafu wote na viraka na jinsi ulivyo.

Kwetu huwa tunakiri tatizo lipo, lakini hutaona tukielekeza vidole vya lawama kwa majirani kiunafiki, tunapambana nalo ndani kwa ndani.

Mkuu, video uliyotuma na kile ulichosema havifanani

Kama huna MB tafuta ukopeshwe kisha itazame video yote mpaka mwisho uone jinsi dhambi ya ubaguzi huwa kwenu japo kimya kimya na kiunafiki unafiki.
 
Usilazimishe matatizo yenu yafanane na ya kwetu.

Angalieni mlipojikwaa,msiangalie mlipoangukia.

Endeleeni kutufuatilia sisi tunasonga tu.

Habari zenu hatuna,zetu mnazo tena zimejaa tele.

Hatuwezi tukafanana maana sisi ni wawazi ila nyie mumekua mabingwa wa kuficha maradhi na uozo kama Korea Kaskazini, janga la Corona limedhihirisha jinsi mlivyo, mnaweza kufanya chochote hata kuacha watu wajifie ilmradi tu msitajwe mna maradhi.
 
Sasa maneno yatalingana kuuwana? Hayo maneno yanatokana na hulka ya mwanadam anapofura, tz huwezi kuta watu wanauwana ajili ya ukabila wala asili.
 
Hawa tushawajua wafichaji data na takwimu.

kuwakandamiza wanahabari ,kuficha maovu na mabaya yanayotokea isijulikane hata kwa wananchi. Nchi inayojiamini ni ya asali na maziwa inaishi kwa uongo, propaganda na misifa.

Kujidanganya hawajui wanajiumiza wenyewe. Hawajitambui, hawajui nchi yao iko level gani, wako comfort zone.

Thats why gap kati yetu inazidi kupanuka huku Wakenya wakiexpose mabaya yao ili kuzitatua na kuhimiza serikali iwajibike
 
Maneno huwezi kulinganisha na nchi yenye watu washamba ambao wanaunganisha vyama vyao vya siasa katika misingi ya ukabila.
 
Kwani kuna kosa gani kumwambia mtu arudi kwao Yemeni kama yeye mwenyewe anasema ni Muyemeni? Unaelewa maana ya Ukabila? Isitoshe kuna tofauti kubwa kati ya kusema/kumwambia mtu, arudi kwao'' na kumfukuza kama vile Wakikuyu walivyofukuzwa Ukalenjinini na mali zao kuharibiwa na kuporwa ndani ya nchi yao wenyewe, huo ndiyo Ukabila, kama ulikuwa haujui maana ya ukabila, Tanzania yetu ni nani kafukuzwa ndani ya Tanzania au kazuiwa asiishi sehemu fulani sababu tu hana asili ya hilo eneo?
 
Bunge ni eneo maalum ambapo kuna Uhuru wa kusema lolote bora linafuata kakuni za bunge. Wala hata ukivunja kanuni hizo, hakuna cha kuwekwa rumande. Labda spika akukumbushe kakuni ama ukizidi sana akufukuze.

Hayo ndio yanayo fanyika kwa nchi za kidemokrasia. Nchi za kijinga ndizo zinapeleka matamko ya kuzingua kwa wananchi na kuwagawa badala ya kuongea hayo bungeni.
 
MK254,

Tanzania wako na Shida ju wamezoea kulamba waarabu matako. Wakenya wamekalia Waarabu na Wahindi lakini watanzania wamekaliwa na Waarabu hadi Mji wao mkubwa ukaitwa Dar es Salaam[emoji23]. Heri hii Nairobi ya Maasai.
 
MK254,

Usilolijua ni sawa na usiku wa Giza , Tanzania kuna makabila Zaid ya 120 kwahiyo kila kabila lina mtani wake tunataniana katika kabila lililona watani wengi wasukuma sasa swali la kujiuluza kama mtu kweli wa Oman kafikaje bungeni kama kweli wewe unayo akili timamu
 
Tanzania wako na Shida ju wamezoea kulamba waarabu matako. Wakenya wamekalia Waarabu na Wahindi lakini watanzania wamekaliwa na Waarabu hadi Mji wao mkubwa ukaitwa Dar es Salaam[emoji23]. Heri hii Nairobi ya Maasai.

Hehehehe!!!
 
MK254,

IMG_20200615_202604.jpg
 
Kwani kuna kosa gani kumwambia mtu arudi kwao Yemeni kama yeye mwenyewe anasema ni Muyemeni? Unaelewa maana ya Ukabila? Isitoshe kuna tofauti kubwa kati ya kusema/kumwambia mtu, arudi kwao'' na kumfukuza kama vile Wakikuyu walivyofukuzwa Ukalenjinini na mali zao kuharibiwa na kuporwa ndani ya nchi yao wenyewe, huo ndiyo Ukabila, kama ulikuwa haujui maana ya ukabila, Tanzania yetu ni nani kafukuzwa ndani ya Tanzania au kazuiwa asiishi sehemu fulani sababu tu hana asili ya hilo eneo?

Nyie mnao ukabila wa namna nyingi tu, sema ni vile mpo vizuri kwenye kuficha. Uchama kwenu ni balaa belua.
Jamaa hapa anapokea matofali kisa kavaa mavazi msiyoyapenda.

2294925_2294894_tapatalk_1578598866010.jpeg
 
Unaelewa maana ya Ukabila? Sasa uchama na Ukabila vina uhusiano gani? Au unafanya makusudi kujaribu kukimbia kivuli chako kinachokuandama kila mahali? Mimi maisha yangu yote sijawahi kushuhudia Ukabila dhidi yangu nchini Tanzania popote pale nilipoishi.
 
Nyie mnao ukabila wa namna nyingi tu, sema ni vile mpo vizuri kwenye kuficha. Uchama kwenu ni balaa belua.
Jamaa hapa anapokea matofali kisa kavaa mavazi msiyoyapenda.

2294925_2294894_tapatalk_1578598866010.jpeg
Unazidi kuchanganyikiwa
 
Kama huna MB tafuta ukopeshwe kisha itazame video yote mpaka mwisho uone jinsi dhambi ya ubaguzi huwa kwenu japo kimya kimya na kiunafiki unafiki.
Team domo vs team hapa kazi tu.
 
Back
Top Bottom