Bunge la Uganda laondoa kikomo cha umri wa kugombea urais

Bunge la Uganda laondoa kikomo cha umri wa kugombea urais

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
_99307000_815e56c4-278d-494e-86d6-33bde3b1dd7d.jpg

Wabunge wa Uganda wameyapitisha mabadiliko ya Katiba ambayo sasa yanamruhusu Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa kwa muhula wa sita.


Baada ya siku tatu za majadiliano mazito na mivutano, hatimaye waondoa ukomo wa umri wa miaka 75 kwa mgombea urais. Wabunge wa upinzani walitoka ndani ya ukumbi zaidi ya mara moja na sita kati yao walifukuzwa ukumbini kutokana na kuupinga muswada. Na hatimaye spika wa bunge hilo Bi Rebecca Kadaga akitangaza matokeo baada ya kupiga kura ya mwisho ikiwa wapiga kura wawili hawakuwa na upande, upinzani wamepata kura 62 na wanaotaka kuondowa kikomo kura 315 na hivyo Spika kutangaza kuwa mswaada huo umepita baada ya kusomwa mara ya tatu.

Wabunge pia wamerejesha ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani kutoka miaka saba hadi miaka mitano, kwa hivyo wabunge wa sasa wataendelea kuongoza hadi mwaka 2023.

Ni pengine kutokanana malalamiko kuwa kuondolewa kwa ukomo wa umri kunaweza kumfanya Bwana Museveni kuwa Rais wa milele. Wafuasi wa Museveni wanadai ni waganda ndiyo wanaweza kumwondoa madarakani kwa Kura

Upande wa upinzani waliweka pingamizi kuzuia mswaada huo usipite lakini idadi yao katika bunge ni ndogo, kiongozi wa wabunge wa upinzani Winne Kiiza amesikitishwa na kupitishwa mswaada huo.

Lakini upande wa chama tawala ulitumia kila mbinu kuona kwamba mswaada huo unapita ili Rais Museveni kuendelea kutawala .

Kupitishwa mswaada huo kunampatia tena Rais Museveni kutawala miaka mingine 14 kulingana na mswaada huo, lakini raia wa Uganda wengi walikuwa hawaungi mkono kubadilishwa kwa katiba kumuongeza Rais Museveni kutawala baada ya kutawala zaidi ya miongo mitatu.


Chanzo: BBC
 
Haha..waganda nilikua nawaona watu wa maana sana...kumbe wapuuuzi tu..
Kwa hali ilivyo Afrika Mashariki ya sasa inapitia ktk wakati mgumu sana....Angalia hali ilivyokua Kenya... Tanzania kwetu ndo hakueleweki..na kuna njemba moja iliishaanza chokochoko za kuongeza muda wa Urais....Waganda ndo hao ......wanaelekea kwenye Udikteta per see...
Bunge la Afrika Mashariki limewaka tayari..kuna watu wamesusia bunge..
Mchawi alieturoga waafrika atakua alikufa miaka 1000 nyuma
 
Haha..waganda nilikua nawaona watu wa maana sana...kumbe wapuuuzi tu..
Kwa hali ilivyo Afrika Mashariki ya sasa inapitia ktk wakati mgumu sana....Angalia hali ilivyokua Kenya... Tanzania kwetu ndo hakueleweki..na kuna njemba moja iliishaanza chokochoko za kuongeza muda wa Urais....Waganda ndo hao ......wanaelekea kwenye Udikteta per see...
Bunge la Afrika Mashariki limewaka tayari..kuna watu wamesusia bunge..
Mchawi alieturoga waafrika atakua alikufa miaka 1000 nyuma
Ongezea na Yale yanayotookea Burundi...wananchi wachangie election costs kwa watumish ukiwa ni lazima jaribu 10% ya salary.
Rwanda na kagame wao.....nae atatawala milele.
Congo na piece instability.... Hata sijui Nani atamshauri mwenzie
 
Naona Afrika,
Maraisi wanavyoambukizana akili za kiu ya madaraka.

Hii akili sijui waafrika wameitoa wapi jamaani.
Mungu tu ndiye atakayeliokoa bara hili la Africa.
 
Hivi kwanini wazungu hawakutuangamiza kwenye vita ya Kwanza na ya pili tufe wabaki wao, naona kama tunawajazia serve hapa duniani.
 
Baada ya kuona umri umesogea kaamua kupunguza toka miaka 7 mpaka 5....!
 
Baada ya hapo, Bongo tujiandae. Mkakati huu unaandaliwa kimyakimya kwa kuua upinzani Tanzania, baada ya hapo mambo yatapitishwa bila kupingwa bungeni.

Ila kwa Kenya huu upuuzi hautatokea, coz watakuwa wameigawanya nchi, make upinzani utapata hoja mpya.
 
Africa kwanini tunatepoza pesa nyingi kwa ajili ya Uchaguzi wakati matokeo yanajulikana miaka na miaka ni yaleyale. Hizo pesa si bora tugawane wengine mshiko wetu tukakae bar tulewe pombe kuliko kuleweshwa politics bila kupenda! [HASHTAG]#MaoniTu[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom