#COVID19 Bunge la Ujerumani laidhinisha ulazima wa chanzo kwa wauguzi

#COVID19 Bunge la Ujerumani laidhinisha ulazima wa chanzo kwa wauguzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Bunge la Ujerumani limepiga kura kuifanya chanjo dhidi ya virusi vya corona kuwa sharti la kisheria kwa wafanyakazi wa sekta ya afya kuanzia mwezi Machi mwaka ujao. Muswada wa sheria hiyo uliowasilishwa na serikali mpya umeungwa mkono kwa kiwango kikubwa na kambi zote za kisiasa.

Kutokana na sheria hiyo, wafanyakazi wa hospitali na wahudumu katika vituo vya wazee watalazimika kuthibitisha kuwa ama wamepata chanjo dhidi ya corona, au wameugua ugonjwa huo na kupona, ili waruhusiwe kuendelea na kazi. Matokeo yanayoonyosha kupimwa na kutokutwa na virusi hivyo, hayatakubalika.

Chini ya sheria hiyo mpya, orodha ya watu wanaoweza kuitoa chanjo dhidi ya corona imerefushwa, wakijumuishwa wafanyakazi wa maduka ya dawa na madaktari wa meno.

Aidha, majimbo 16 ya Ujerumani ambayo ndiyo yenye dhamana ya sera ya afya, yatakuwa na nguvu zaidi kuhusiana na Covid-19, ikiwemo uwezo wa kuamuru vituo kufungwa.
 
Back
Top Bottom