Bunge la Ukraine laidhinisha mpango wa kusajiliwa wafungwa jeshini

Bunge la Ukraine laidhinisha mpango wa kusajiliwa wafungwa jeshini

LINGWAMBA

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2023
Posts
484
Reaction score
1,214

Screenshot_20240514-154118.jpg

Bunge la Ukraine limepasisha muswada wa sheria inayoruhusu kukusanywa na kusajiliwa jeshini wafungwa wa nchi hiyo.

Tovuti ya habari ya Russia Today imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, rasimu ya mwisho ya muswada huo ilipigiwa kura kwa wingi bungeni jana Jumatano baada ya kufanyiwa marekebisho ya hapa na pale.

Serikali ya Kiev ipo mbioni kusajili wanajeshi, baada ya nchi hiyo kupoteza mamia ya maelfu ya askari wake katika vita na Russia tokea mwaka 2022.

Wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Russia, Sergey Shoigu, alisema Ukraine imeshapoteza karibu askari wake nusu milioni tangu Februari 2022 hadi sasa, na kwamba mwaka huu pekee, nchi hiyo imepoteza wanajeshi 111,000.
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Denis Malyuska amekuwa akishinikiza kusajiliwa jeshini wafungwa hasa ambao walipatikana na hatia ya makosa ya jinai.

Wanajeshi wa Ukraine katika medani ya vita

Screenshot_20240514-154205.jpg


Amewahi kusema katika mahojiano na shirika moja la habari kuwa, "(Wafungwa) ambao wamewahi kufanya mauaji huko nyuma, wanaweza kuwa wapiganaji wazuri katika medani za vita."

Kiev imeazimia kuunda vikosi maalumu vya jeshi vitakavyojumuisha wafungwa walioachiwa huru. Viongozi wa Ukraine wanasisitiza kuwa, jeshi la nchi hiyo limepata vipigo katika medani za vita kwa kutopewa msaada wa kutosha wa kijeshi na Marekani na waitifaki wake.

 
Hii nchi sijui baada ya vita itabaki na watu gani, maana inaonekana wanaume woye wapo vitani, au wamekufa!

Na wale waliokimbia nje ya nchi wanasakwa kila sehemu ili warudi kutumikia jeshi.

Inaonekana wamepoteza watu wengi sana, sijui kama jeshi lao linaweza kuendelea na vita kwa miaka mingine miwili.
 
Yale yale ya urusi kutumia wafungwa vitani...!
 
hii nchi sijui baada ya vita itabaki na watu gani, maana inaonekana wanaume woye wapo vitani, au wamekufa!

na wale waliokimbia nje ya nchi wanasakwa kila sehemu ili warudi kutumikia jeshi,.....

inaonekana wamepoteza watu wengi sana, sijui kama jeshi lao linaweza kuendelea na vita kwa miaka mingine miwili....
Putin kawa pukutisha sana. Western countries wanatoa siraha wakati hakuna watu wa kuzitumia barabara. Vijana wengi wamekimbia nchi. Kuna sera ime anzishwa huko kama kwenda JKT kwa mujibu wa sheria huku kwetu, hao wamefyekwa sana. Kuna maadaano ya akina mama kila siku Kiev wakiitaka serikali iache sera hiyo.
 
Wafungwa Kwa makosa ya jinai, Toka lini wakawa wazalendo wazuri Kwa Nchi,
NB,Kukaa mezani kufanya diplomacy, Vita Sio suluhisho la matatizo
 
Hao maraia mwanzoni kabisa mwa vita walijitolea kwa wingi sana kiasi kwamba mpaka wabibi walikuwepo

Kumbe walifyekwa wote
 
Kila mtu lazima apiganie nchi yake, hongereni watu wa Ukraine...haiwezekani uvamiwe kwako na panga alafu unyoshe mikono juu. Mwisho uanzisha mwanzo
 
Wafungwa Kwa makosa ya jinai, Toka lini wakawa wazalendo wazuri Kwa Nchi,
NB,Kukaa mezani kufanya diplomacy, Vita Sio suluhisho la matatizo
Papa alimwambia , wajifanya wajanja
 
Hii nchi itakuja kukosa rasirimali watu maana imeamua kuwaacha wapukutishwe. Na urusi haina haraka ni mdogo mdogo mazishi ni kila siku
 
Back
Top Bottom