Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Imeelezwa na chombo hicho cha kutunga sheria kuwa fedha hizo zilichotwa katika biashara ya uendeshaji wa machinjio ya Dodoma katika kipindi cha miaka 11 iliyopita.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa, amesema wamebaini watendaji wa Narco na Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliohudumu katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2015, walishirikiana kwa pamoja na Kampuni ya Nicol kuwaibia Watanzania fedha hizo, akisisitiza kuwa Bunge la 11 kamwe haliwezi kubariki wizi huo.
Alitoa agizo hilo alipozungumza kwenye ziara ya kamati hiyo kutembelea machinjio ya Dodoma ambayo kwa sasa yanaendeshwa na serikali baada ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, kuvunja mkataba huo baina ya Narco na Nicol ulioingiizia hasara serikali kwa kipindi cha miaka 11, huku wahusika waliohusika na kashfa hiyo wakiwa bado hawajachukuliwa hatua yoyote.
Mgimwa alieleza kushangazwa na usimamizi mbovu, ubadhirifu na ukiukwaji mkubwa wa mkataba wa uendeshaji wa machinjio hayo, akihoji uadilifu wa watendaji waliopewa dhamana kusimamia mali hiyo kwa niaba ya Watanzania.
Alihoji iweje tangu mwaka 2008 ufisadi huo umefanyika bila wahusika kuchukulia hatua wakiwamo waliokuwa watendaji wa Narco, Nicol na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, hivyo akaitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwatafuta na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Kamati hiyo ilipongeza uamuzi wa serikali kuvunja mkataba wa mauzo ya mali za machinjio hayo baina ya serikali na Kampuni ya Nicol na kuyarejesha machinjio chini ya umiliki wa serikali na kuitaka kufanya haraka kurejesha masoko ya nyama katika nchi za Falme za Kiarabu yaliyopotea kutokana na usimamizi mbovu wa waendeshaji hao wa zamani.
Pia iliitaka serikali kuhakikisha fedha zote kiasi cha Sh. 9,712,127,660 (Sh. bilioni 9.7) zilizoibwa katika biashara ya machinjio, zinalipwa haraka pamoja mbia Nicol kulipa madeni yote inayodaiwa Kampuni ya Ubia TMCL kiasi cha Sh. bilioni 5.248.
Licha ya kupongeza uamuzi wa Narco, ambaye ni mbia katika Kampuni ya Ubia TMCL kujiondoa kwenye ubia huo, kamati hiyo ilisema bado kuna haja viongozi waliohusika na ufisadi huo kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Mbunge wa Moshi Vijijini, Antony Komu, alisema uamuzi uliofanywa na Waziri Mpina katika kubaini kasoro hizo na kuchukua hatua, unapaswa kuendelezwa kwa serikali kutengeneza mfumo endelevu wa kubaini udhaifu na kuchukua hatua, akisikitika kuona ufisadi mkubwa kiasi hicho umefanyika pasi na wahusika kuchukuliwa hatua.
Komu alitaka hatua kama hizo ziwe endelevu ili kunusuru mali za nchi badala ya kumwachia kiongozi mmoja tu ambaye ni Waziri Mpina kusimamia mambo kama hayo.
Mpina aliihakikishia kamati hiyo kuwa serikali iko kwenye hatua ya mwisho za kufanya ukarabati mkubwa wa machinjio hayo na kurejesha upya masoko ya nyama nje ya nchi, ikiwamo nchi za Famle za Kiarabu na Comoro.
Pia, aliihakikishia kamati hiyo kuwa wote waliohusika na wizi na ubadhirifu, hawatapona kwa kuwa serikali inajua kuwa mbali na fedha hizo zilizoibwa, hata mishahara ya wafanyakazi wa kampuni hiyo nayo ilifanyiwa ufisadi na kuleta usumbufu mkubwa kwa watumishi.
Waziri Mpina alisema kwa muda mrefu Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kurekebisha kasoro za uendeshaji wa Machinjio ya Dodoma kama sharti muhimu katika mkataba wa mauzo ya mali kwenye Ibara ya 4.1.3.1 na kwa kuwa jitihada za kuinusuru Machinjio hiyo zimefanyika kwa muda mrefu bila ya mafanikio yoyote.
Alisema serikali ilijiridhisha kwamba mbia (Nicol) amekiuka vipengele muhimu vya mkataba katika ibara ya 7, 13, 6, 9 na 102; Pia Nicol imekuwa ikifanya biashara na mali za kampuni bila ya kuwekeza na bila ya kutoa gawio kwa serikali kwa kipindi chote cha miaka 11 iliyokabidhiwa kiwanda hicho.
Waziri Mpina amesema tangu machinjio hiyo ibinafsishwe, serikali imeendelea kupata hasara na mali nyingi za kampuni kama mitambo, majengo, magari na rasilimali nyingine zimechakaa na hakuna ukarabati wowote uliofanyika.
Pia nchi yetu imepoteza ajira, fedha za kigeni, biashara na masoko ya mazao ya mifugo baada ya kiwanda kufungiwa kuuza mazao ya mifugo katika nchi za Jumuiya ya Kiarabu (UAE).
Alisema kampuni 10 pia zilisimama kusafirisha na kufanya biashara ya nyama baada ya kiwanda kufungiwa ambapo kwa mwezi mauzo ya nyama nje ya nchi katika machinjio yalikuwa yamefikia tani 192 sawa na mbuzi 24,000. Pia kiwango cha uchinjaji wa ng’ombe kushuka kutoka wastani wa ng’ombe 120 hadi 50 kwa siku.
Alibainisha kuwa hasara na madeni ya Kiwanda cha TMCL yanaendelea kukua kila uchao huku mbia (Nicol) akishindwa kurekebisha kasoro zilizobainika katika vipindi tofauti hata baada ya kupewa notisi ya muda wa siku 30 na hata mbia mwenzake (Narco) kumpa notisi ya siku 180.