Bunge lakumbwa na kashfa nzito


kwanza si vyema kutaja majina ya watu bila idhini japokuwa unahoja. Pili kuitwa interview watu wa darasa moja siyo ajabu, mimi nilifanya interview pale TBL DSM mwaka 2006 na alikuwa anatakiwa maintenance engineer tukakutana watu tisa wote darasa moja na mmoja wetu akachukuliwa. Nadhani acha vijana wenzetu wachape kazi cha msingi wasijiingize kwenye ufisadi.
 

Naona mnapteza DIRECTION mmeacha mada mnakimbilia mabishano ya VYUO. UDSM au what what kama iko juu ni kwa kila IDARA? Acheni habari hizo jamani.
 

Majina tayari yapo kwenye public domain na hakuna siri kwa sababu yalishawekwa wazi mpaka magazetini

hivi umeelewa hii scandal ilivyoanza au ndio unarukia tuuu?
 

malalamiko hayana hoja kabisa.Na kuna kipindi TANESCO walichukuwa watu 29 wa advanced diploma wakawapiga chini jamaa wa udsm nao walilalama hivi hivi ila sema kipindi hicho mitandao ilikuwa sio maarufu sana.Ukiwauliza kwanini wanalalama eti kwa sababu wao ni udsm.

Lakini ikitokea wa udsm wamechukuliwa wengine wameachwa hutosikia kelele hizi.Wao watuambie tatizo ni lipi? kwa sababu walioachwa ni udsm na tumaini ama kwa sababu walioitwa wana diploma hawana digrii.
 
hili naona ni tatizo mkuu mimi sioni kama kulikuwa na mkataba lazima watu fulani kutoka ktk chuo fulani lazima wawepo ktk shortlist.Labda wewe nieleze kidogo ni kivipi hao jamaa wamezulumiwa.

ungeuliza swali hili hapo awali kweli ningekuona una nia ya kutaka kujua kiini cha hii issue

tatizo uliamua kuivamia kichwa kichwa sasa inavyoelekea hukujua issue hii ikoje

je unajua hii issue ilianzaje mpaka ikafika hapa ilipofikia?
 
Wakuu,

Hii hoja ina mambo mengi sana na ngumu kuchangia bila kujikanyaga. Kuna mambo mengi yamejadiliwa na mengi yanapingana.

Je ni lazima kuweka chuo ulichosoma kwenye kila CV? Hapana sio lazima ila ni muhimu. CV ni picha ambaye unampelekea dada anayetaka kuchagua mume wa kumuoa. Sifa za kuwa mume bora ziko nyingi sana na katu haziwezi kujulikana kwa kutumia hii picha moja. Lakini utakuwa kichaa kama utatuma picha ambayo unaonekana ni kituko. Inategemewa kwamba utajaribu kupeleka picha nzuri zaidi ili angalau uwe kwenye shortlist ya kuonana na huyu dada na hapo ndipo sifa zingine zitajulikana.

Chuo ulichosoma kinasaidia kuonyesha/kutoonyesha sifa uliyonayo. Kwa kutokuweka jina la chuo unaweza kuonekana umeficha makusudi, hivyo hufai, unaweza kumpa hamu huyo mtu atake kujua zaidi juu ya wewe na hivyo kukuingiza kwenye shortlist.

Kiujumla nitasema kwa kazi ambayo ni professional, nategemea kuona jina la chuo ulichosoma. Ukisema umemaliza form four lazima useme umemaliza wapi? Ukiandika umemaliza chuo kikuu, nitategemea useme ni chuo gani.

Kwa wengine chuo ulichosoma na kupasua kwako vinaishia kwenye shortlist. Ukija kwenye interview nitataka zaidi kujua unajua nini. Kila mtu ninayemwita kwenye interview ninakuwa na uwezo wa kumpa kazi. Ni kwamba katimiza minimum requirements ya kazi husika. Kwahiyo kuniambia umemaliza na A+ hainisaidii, ninataka kujua shuleni umefanya nini, umefanya projects zipi, mwisho wake ulikuwaje, ulipambana na matatizo gani, uliyatatua vipi nk. Mtu ninayempa kazi ni kwasababu amenionyesha anajua nini.

Je inawezekana kuchukua wanafunzi wa chuo kimoja tena darasa moja? Ningelikuwa mimi nisingelifanya hivyo hata siku moja hata kama hicho chuo kingelikuwa bora sana. Diversity ni jambo muhimu sana, kwa kuwa na interviewees toka vyuo mbalimbali unaweza kujifunza mengi na hivyo kufanya uchaguzi ambao ni wa maana zaidi. Hata probability inakataa kwamba katika vyuo 10, chuo kimoja tena watu wa mwaka mmoja wanaweza kuwa wazuri kuliko hawa wengine wote.

Haya mambo ya chuo kipi bora, nafikiri yapo toka miaka na miaka. Nakumbuka wakati wengine tupo mlimani, kulitokea vita kali kati ya UDSM na Mzumbe. Mwenyekiti wetu alitamka kwenye vyombo vya habari kwamba inakuwaje wanafunzi wa junior colleges kama Mzumbe wapate allowances kubwa kuliko sisi. Mzumbe walikuja juu sana.

Sidhani kama mijadala kama hii inasaidia sana jamii. Uzuri wa jambo unatokana na mambo mengi sana. Inawezekana UD ni brand kubwa na inapata wanafunzi wengi wazuri kwasababu ya jina lakini je output yake pia ni nzuri? Ni vizuri kumwangalia kila mtu individually na kumpima kama anafaa au la. Tukianza kuajiri watu kwa kufuata amesoma wapi, inaweza kutuletea matatizo mengi sana.

Kuitwa kwenye interview ni hatua kubwa kuelekea kupata kazi. Ukisoma chuo ambacho brand yake inajulikana unakuwa umejirahisishia njia ya kwenda kwenye interviews nyingi na hivyo kupata kazi kirahisi. Chuo kikiwa na brand kama vile Oxford, Havard nk. kinakuwa kinapata wanafunzi wazuri zaidi, kinavutia walimu wazuri zaidi, research nyingi muhimu zinapelekwa kwao, ni rahisi kupata pesa nyingi zaidi, hivyo mara nyingi hata output yake inakuwa graduates wenye uwezo zaidi.
 
Kwa habari nilizonazo toka ndani ya Bunge, hizi kazi waliapply watu zaidi ya 2000. Inakuwaje wachaguliwe watu wa chuo kimoja, same intake tena wasio na uzoefu kama kweli hicho kilikuwa ni moja ya vigezo?

Hao wanafunzi, kama habari ni za kweli, wametoka kwenye chuo chenye harufu ya udini, kutokana na jina la chuo kilichotajwa, wa-Islam tukisema ''bunge halifati sheria lina fata udini'' tutakuwa tumekosea? nina shaka kuwa hao short listed candidates watakuwa 95% waKiristo kama si mia kwa mia na kuna sababu tosha (chuo kilichotajwa) kuwa hakuna hata mmoja muIslam.

Tuendelee, tutafika tu.
 



Kwa habari nilizonazo toka ndani ya Bunge, hizi kazi waliapply watu zaidi ya 2000. Inakuwaje wachaguliwe watu wa chuo kimoja, same intake tena wasio na uzoefu kama kweli hicho kilikuwa ni moja ya vigezo?

Hivi MkamaP unajua unajikanganya na maandishi yako. Mara unasema kuwa wajanja hawaangalii ufaulu wako, mara nenda na first class yako na andika CV yako shaghalabaghala nenda kwenye interview ushindwe kuwakilisha uone jinsi utakavyopigwa bao na watu wa third class. Hawa toka vyuo vingine hawajaitwa kwa interview, ingekuwa katika hizo nafasi saba wameita watu 10 toka SAUT, 8 toka Tumaini, 9 toka Mzumbe na 7 toka UDSM, then baada ya interview wakapata wote wa SAUT hapo kidogo ina sound, lakini kuwatoa wote karibia watu 2,000 kuwa hawana vigezo walivyo navyo watu toka darasa moja huo ni kuleta kujuana, kuangalia maslahi nk.

Pia unapojikanganya ni hapa unapozungumzia kutoweka sehemu uliyosoma, kama vile uliangalia CV za hao walioitwa, hapa unatoa mawazo yako unayohisi yanasaidia ukiwa unaapply kwa kazi fulani. Na kutoweka kwenye CV kuwa ulipata wapi degree inaweza kuwa chanzo vile vilecha kutoitwa kwa interview kama wengine watakuwa wameweka.

Mjadala na kinachoshangaza ni watu zaidi ya 2,000 kama data zilivyotolea, then karibia watu wote 15 watoke chuo kimoja (SAUT) na wote walimaliza darasa moja. Hii haiwezekani hata kwa ufikiri mdogo tu, yani unataka sema wote waliobaki walikuwa hawana vigezo kabisa zaidi ya hawa wa chuo kimoja. Ni sawa vile vile kama hawa watu wangetoka darasa na chuo kimoja kama UDSM, MU, Tumaini, Oxford, Cambridge nk. Nayo tungeuliza, wote wawe chuo kimoja na darasa moja haiwezekani. Hivyo wanaosema UDSM ni bora zaidi ya
 
Dowans Vs Ndege ya Rais(aka. Air Majani or Air Mramba) Hivi kina Mwakyembe hawakujua Air Mramba ni mtumba? au mtumba ni mitambo tu
 
waacheni wafu wazike wafu wao

Mkuu fafanuwa kidogo wafu ni wepi? Maana kama unamaanisha wafu ni hao wahitimu wa AUG sielewi kabisa.

Maana wanaloliangamiza na kulimeng;enyuwa taifa hili kwa 99.999999% wanajulikana ni wahitimu wa chuo gani.

Dhama za kuangalia chuo gani unatoka zimepitwa na wakati ,waajili wanaangalia nini unakifahamu na utaweza kudili sawasawa na kuongeza tija zao ktk utendaji wa taasisi yao.

Mtu anakuja na tuhuma za udini hii naiona imekaa kimaajabuajabu ,maana mtu kama ni udini unaweza chukuwa watu kutoka kokote kule duniani na bado ukachukuwa wa dini moja.

Hoja ni ipi hapa sielewi? kama umeweka mtihani na unataka ili apasi anafikisha maksi fulani na kwa bahati nzuri zikafikishwa hizo maksi na watu wa familia moja utawaacha uchukuwe waliofeli eti kwa sababu wametoka familia moja.

Mfano wasaili ili wakupe kwenda stage ya pili wanaangalia muundo wa CV, mambo yaliyomo ndani, lugha jinsi iivyotumika yani usahihi wa lugha maana hii kazi inaendana na lugha kiswaz ama kiigereza na mwisho wanatowa maksi ktk CV ,cv zilizofikia maksi fulani ndio zinaingizwa stage ya pili ,sasa kama jamaa wamefeli mnataka waingizwe ndani ??

Kitu kingine mnaweza kuwa mmesoma kozi moja lakini baadhi ya masomo mmetofautiana na wengine hawakuyasoma kabisa, sasa je kama mwaajili anataka jamaa wawe na uelewa ktk eneo fulani sasa ninyi kwa bahati mbaya hamkusoma hicho kitu si mnapigwa chini wote.

Mfano mwingine tuseme wizara ya mambo ya nje inaajiri wafanyakazi sasa ndani za creteria zao inakuwa cv inayopita lazima awe anafahamu lugha tatu za kigeni kwa bahati nzuri ama mbaya ST Aug wakawa wanafundisha Kichina na kispanish ,harafu ninyi udsm ni kiigereza tu ,mkija mkapigwa chini mnalalama eti watu wa chuo kimoja wamechukuliwa???

Hapa narudia tena kuomba taarifa mwenye nazo tatizo ni kwasababu udsm wamepigwa chini ama kwa sababu AUGST hawawezi kuitwa wakachwa chuo BABU K udsm.?
Kama tatizo ni Rushwa basi tulpeni hizo detail tutasambue mambo
 
 
tatizo ni kuwa kuna irregularities zilitokea wakati wa zoezi hili sasa waliochemsha hawakujua kama issue itafikia hapa ilipofikia

kama wangekuwa na akili walitakiwa kulisort out as soon as possible lakini its too late now
 
 
Bunge mradi wa ulaji

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAKATI baadhi ya wabunge wakiendelea kulumbana kupitia katika vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali yanayogusa maslahi ya taifa, imebainika wamekuwa wakichuma mamilioni ya fedha kupitia katika malipo yao halali ya mishahara, posho na fedha nyingine zisizotokana na malipo yao rasmi wanayostahili.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano umethibitisha pasipo shaka kwamba, fedha ambazo wabunge wamekuwa wakichuma kwa njia mbalimbali kwa kutumia nafasi zao za uwakilishi, zinaweza zikawa sababu mojawapo muhimu ya kuibuka kwa makundi yanayosigana ndani ya Bunge na hususan miongoni mwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, gazeti hili limefikia hatua ya kutilia shaka kwamba, mzozo wa hivi karibuni, kati ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe na mwenzake wa Igunga, Rostam Aziz, kwa kiwango kikubwa unakuzwa kutokana na sababu za maslahi binafsi zaidi kuliko madai ya uzalendo na maslahi ya taifa.

Shaka hiyo ya Tanzania Daima Jumatano inatokana na ukweli kwamba, wabunge hao wawili ambao wote wawili ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwa namna moja au nyingine wamepata kuwa au wanayo maslahi ya wazi na ya moja kwa moja katika sekta ya nishati.

Kauli ya hivi karibuni ya mmiliki wa Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, Mohammed Al Adawi, kukiri kwamba aliwekeza katika sekta ya nishati kwa ushawishi wa Rostam sambamba na ile ya kubainisha kuwa kampuni ya mbunge huyo ilipata kuingia katika zabuni ya kutaka kufanya kazi za ujenzi katika mradi wa kuzalisha umeme wa dharura, ni ushahidi wa wazi wa namna mwanasiasa huyo alivyo na maslahi ya moja kwa moja katika sekta ya nishati.

Kama ilivyo kwa Rostam, taarifa za hivi karibuni, zilizothibitishwa na Mwakyembe mwenyewe kuwa ni mmoja wa wakurugenzi waanzilishi wa Kampuni ya Power Pool East Africa Ltd yenye malengo ya kuzalisha umeme wa upepo kutoka mkoani Singida, ni ushahidi kwamba naye anayo maslahi ya moja kwa moja katika sekta ya nishati.

Kuingia kwa Rostam na Mwakyembe katika sekta ya nishati, kwa kiwango kikubwa kunaonyesha namna wabunge, hususan wale wa CCM walivyojizatiti kutumia fursa zao za kisiasa kujinufaisha kiuchumi, nyuma ya kivuli cha uwekezaji kupitia sheria ya soko huria.

Kama hiyo haitoshi, mzizi wa fitina kuhusu ukweli kwamba Bunge limekuwa likitumiwa kama kiota cha wanasiasa kuvuna mamilioni, zilithibitishwa mkoani Kilimanjaro juzi na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibrod Slaa ambaye alisema mshahara anaolipwa mbunge kwa mwezi unafikia sh. milioni saba, hiyo ikiwa mbali na posho nyingine.

Dk. Slaa alitaja kiwango hicho cha mshahara wake wakati akihutubia wakazi wa mji mdogo wa Hedaru, wilayani Same katika mfululizo wa mikutano ya Operesheni Sangara inayoendeshwa na CHADEMA.

Wakati Dk. Slaa akibainisha ukweli huo, uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano umebaini pia kuwa wabunge wanaweza kujikusanyia mamilioni ya shilingi kwa kuhudhuria vikao mbalimbali vya kamati za kudumu za Bunge, semina na safari za ndani na nje ya nchi.

"Ndugu zangu, afadhali msijue mshahara anaolipwa Dk. Slaa kama mbunge, mkijua nalipwa shilingi ngapi mnaweza hata kunipiga mawe," alisema Dk. Slaa wakati akihutubia mkutano huo na kuitikiwa na sauti za wananchi wakimtaka ataje mshahara wake.

"Mnataka kuujua mshahara wangu, ninalipwa sh milioni saba kwa mwezi. Haki iko wapi? Mimi nalipwa milioni saba, na posho yangu kwa siku ni sh 135,000. Haya ni malipo makubwa mno, fedha ninayopata kwa siku inaweza kuzidi hata mshahara wa mwezi mzima wa polisi. Muulizeni yule polisi pale analipwa shilingi ngapi msikie.

"Juzi nimetaja posho za wabunge na kusema zipunguzwe, lakini Spika wa Bunge analalamika eti naingilia haki na madaraka ya Bunge, sasa leo nasema ninalipwa jumla ya shilingi milioni saba kwa mwezi, acha posho za bungeni. Kweli hii ni haki?" alisema Dk. Slaa.

Alisema kuwa akiwa raia huru, ana haki ya kutaja kwa hiari yake kiwango cha mshahara wake, hasa pale anapoona kuwa kulipwa kiwango hicho ni kutowatendea haki mamilioni ya Watanzania maskini wanaolipa kodi zao wakitegemea serikali iwakomboe kutoka kwenye lindi la umaskini.

Dk. Slaa alisema wabunge wengi wa CCM akiwamo Spika wa Bunge, Samuel Sitta, hawawezi kuunga mkono hoja hiyo kwa vile wapo bungeni kwa ajili ya kutafuta maslahi yao binafsi.

"Wafanyakazi wengi na Watanzania wanateseka kwa mishahara midogo na maisha duni, mamilioni haya ya fedha kwenda mifukoni mwa watu ni aibu kwa nchi na CHADEMA tunasema hapana, fedha hizi ziende katika masuala ya kusaidia jamii na kuongeza mishahara ya walimu, polisi, mahakimu na watendaji wengine," alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa na mamia ya wakazi wa Hedaru waliohudhuria mkutano huo.

Alirejea kauli yake ambayo amekwishakaririwa akiitoa mara kadhaa kuwa Spika Sitta, anapaswa kujiuzulu nyadhifa alizonazo katika CCM, ili awe huru kuliongoza Bunge kwa maslahi ya Watanzania badala ya kushinikizwa na maslahi ya chama chake.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, kushangazwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kuendelea kuwateua wabunge wa CCM kuwa wajumbe katika bodi za mashirika ya umma.

Akizungumza wiki iliyopita katika mkutano uliondaliwa na Jukwaa la Wahariri, Prof. Lipumba alisema, hatua hiyo ya Rais Kikwete mbali na kuwahalalishia wabunge ulaji, inazoretesha utendaji wao katika kuyasimamia ipasavyo mashirika hayo ambayo utendaji wake wa kazi unapaswa kusimamiwa na taasisi hiyo muhimu ya dola.

Wakati hali ikiwa hivyo katika mishahara ya wabunge, Tanzania Daima Jumatano limebaini kuwa wabunge wamekuwa wakilipwa mamilioni ya fedha wakati wanapokutana na baadhi ya taasisi za umma ambazo kamati za Bunge zinazisimamia shughuli zake.

Taarifa za hivi karibuni ambazo gazeti hili limezipata zinaonyesha kuwa, Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco) lilitumia jumla ya sh milioni 16 kwa ajili ya kulipa posho na usafiri wabunge kutoka majimboni mwao, pamoja na makatibu wawili waliohudhuria kikao cha dharura kilichowakutanisha Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Kamati ya Bunge ya Kamati ya Nishati na Tanesco.

Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya Bunge, zinaeleza kuwa licha shirika hilo kuwa na hali mbaya kifedha, lililazimika kuingia gharama hizo baada ya ofisi ya Bunge kuitaka Wizara ya Nishati na Madini kuwagharamia wabunge hao kwa sababu Bunge halikuwa na fedha katika kikao chake cha Desemba mwaka jana.

Katika hali ya kushangaza, habari za wanakamati hao wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kulipwa posho na gharama zao nyingine na Tanesco wakati wakihudhuria kikao hicho zimewafanya wabunge, Katibu wa Bunge na Spika kutofautiana.

Spika Sitta, jana alilithibitishia Tanzania Daima Jumatano kuwa, wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini walilipwa posho na gharama za usafiri kwa sababu Bunge halikuwa na fedha wakati Waziri wa Nishati na Madini, Ngeleja alipotaka kukutana na kamati hiyo ili kupata ushauri.


"Lolote linaweza kutokea kutegemea na nani amewaita, kama wameitwa kusaidia jambo ambalo halimo kwenye utaratibu wa Bunge wanalipwa na aliyewaita. Na katika hili ilikuwa hivyo, ninalifahamu vizuri sana, waziri aliomba kukutana na kamati wakati muda wa Bunge ukiwa umepita, Katibu wa Bunge alimuandikia akimueleza kuwa Bunge halina fedha ila kama wizara yake inaweza, basi ilipe posho na gharama za wabunge hao kusafiri hadi Dar ili aweze kukutana nao.

"Hivyo ndivyo ilivyokuwa, sasa mimi sijui kama ililipa wizara, Tanesco au nani, la msingi hawakulipwa na Bunge, na kama wabunge ambao ni wanakamati wanakanusha hili, ni watu wa ajabu kwa sababu sijui wanaogopa nini kueleza ukweli," alisema Spika.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo (CCM), alipozungumza na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani, alikana kupokea senti tano kutoka Tanesco wakati wakihudhuria kikao hicho na kueleza kuwa, kamati yake iliitwa na Spika na malipo yalifanywa na Bunge.

"Hatukumuomba mtu hela, sielewi lolote, sisi tuliitwa na Spika na malipo yetu yalishughulikiwa na Bunge," alisema Shellukindo na kusisitiza kuwa, kanuni za Bunge zinaeleza wazi kuwa wabunge wanapokuwa katika vikao vilivyo na baraka za Spika, iwe bungeni au nje ya Bunge, posho na gharama zao nyingine zinalipwa na Bunge na si taasisi nyingine yoyote.

Alipoulizwa kuhusu hilo, Waziri wa Nishati na Madini, Ngeleja alieleza kuwa Tanesco ililazimika kulipa gharama hizo kwa wabunge licha ya kikao hicho kufanyika kwa ridhaa ya Spika, baada ya Bunge kueleza kuwa halikuwa na fedha kwa ajili ya kulipa posho na gharama za usafiri kwa wabunge.


Wakati wanasiasa hao wakivutana kuhusu mfumo huo wa ulipaji posho, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, alipotafutwa na Tanzania Daima Jumatano ili kutoa ufafanuzi wa jambo hilo, alieleza kuwa wabunge wote wanapokuwa katika shughuli za Bunge, ikiwamo vikao vya kamati za kudumu za Bunge, posho na gharama zao nyingine zinalipwa na ofisi ya Bunge, na si vinginevyo.

Alisisitiza kuwa, Tanesco haiwezi kuliwalipa posho wabunge wakiwa katika kikao cha kamati ya kudumu ya bunge na kuongeza kuwa katika utumishi wake ndani ya taasisi hiyo, hajawahi kuona fedha za Tanesco zikitolewa kwa ajili ya kulipa posho wa wabunge.
 
 
 

Kuvunjwa sheria au kanuni sio kuhalalisha uovu au uzembe.kwenye ajira kuna Diversity na Equal opportunity policy.sawa na unapoenda kuoa kabila lingine unaweza kuingiza vitu vingine lakini mkiwa mnaoa kabila moja tu kuna vitu vingi mtashindwa kuvijua kama weakness.kama TBL walifanya hivyo basi ni kina Kashishilah wengine hao,watu wasiojua taratibu za kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…