Bunge laridhia Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya SADC ya Mwaka 2012

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Bunge la Tanzania Agosti 31, 2023 limeridhia Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) ya Mwaka 2012 ambapo pamoja na mambo mengine, itaondoa vikwazo vya kikodi na visivyo vya kikodi kwa wafanyabiashara wa Tanzania katika nchi za jumuiya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Bunge, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuridhiwa kwa itifaki hiyo kutatoa nafasi ya Tanzania kukuza biashara na kutumia huduma za biashara kwa urahisi zaidi.
 
11 years late!
 
Tangu mwaka 2012! Ilipotea ofisini? Kwa hali hii tusishangae kwanini Indonesia imetuacha mbali sana, sisi ni wazembe.
 
Serikali ya kizembe sana! Hoja ya Mpina inahitaji majibu fasaha kutoka serikalini kwa nini itifaki inaridhiwa miaka 11 baada ya kutolewa? Nini kimechelewesha? Je kuna maboresho yo yote yamefanywa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…