Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Moja ya habari kubwa za sasa hivi nchini Tanzania ni Lazaro Nyalandu ambae juzi ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini.
Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.
Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapo juu..
Hii hapa Barua ya Nyalandu aliyomuandikia Spika