Moja ya habari kubwa za sasa hivi nchini Tanzania ni Lazaro Nyalandu ambae juzi ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini.
Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.
Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapo juu..
Hawa wameshanganyikiwa kabisa bora wangekaa kimya waulizeni hiyo barua kutoka kwa katibu mkuu ikimueleza spika kumvua Ubunge na kwa kikao kipi PolePole asiropoke wakati wa press yake juzi?
Akili ya kawaida nilitegemea kuona barua kutoka ofisi ya katibu mkuu CCM ikieleza kufukuzwa kwa Nyalandu ndipo ifuate ya Spika wamechemka
Picha Lazaro Nyalandu leo akiwa na Tundu Lissu hospital Nairobi leo.