KiuyaJibu
JF-Expert Member
- Aug 29, 2007
- 848
- 191
"Kwenye suala la Bunge, Bunge letu ni kubwa ukilinganisha na wafadhili wetu (Marekani inatufadhili, India inatufadhili nk), sisi Tanzania tuna watu milioni 60+, Marekani ina watu milioni 350+ lakini Bunge lake lina watu 535 Kwa maana ya kwamba Mbunge mmoja wa Marekani anawakilisha watu karibu 700,000 hapa kwetu (Tanzania) hao Wabunge 393 (ukijumlisha na Wabunge wa Viti maalum, Wabunge wa kutoka Baraza la Wawakilishi na Wabunge wa Kuteuliwa na Rais) hata kama kila mmoja angekuwa anawakilisha wananchi (Wabunge wa majimbo) angekuwa anawakilisha watu 150,000 ukilinganisha na hawa wanaotupa fedha (wafadhili) Marekani kwa mfano Ina maana kwamba Mbunge mmoja wa Marekani anawakilisha watu wengi mara tano (5) zaidi ya Mbunge wa Tanzania" -Dkt. Ananilea Nkya
Ni sehemu ya yale aliyozungumza Dkt. Ananilea Nkya wakati akitoa mada kwenye kongamano la Katiba lililofanyika Monarch Hotel, Juni 29.2024, jijini Mwanza
Swali la msingi ninalojiuliza hapa, kwanini tunatumia fedha nyingi kuendesha bunge kuliko nchi zinazotupatia misaada ili hali kuna miradi ya maendeleo inakosa fedha na mingine tunashindwa kuitekeleza kila mwaka.
Nawasilisha kwenu wadau ili tutafakari pamoja ili tuone nini kifanyika.