Mtumishiwetu
Senior Member
- Jul 13, 2022
- 196
- 346
Nimefuatilia mjadala mkubwa wa Waziri wa Nishati kutumia lugha za kashfa kwa Mamlaka iliyokuwa inahoji kuhusu kuchelewa kwa Bwawa la Julius Nyerere pamoja na tatizo la kukatika kwa umeme.
Sote tunatambua hoja hizo ziliibuliwa bungeni na Kamati za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambayo na yenyewe zililalamikia tatizo la kukatika kwa umeme namna lilivyoathiri uzalishaji viwandani.
Rejea,
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA YA KAMATI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA (FUNGU 44) KWA MWAKA 2021/2022 PAMOJA NA MAONI YA KAMATI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FUNGU 44 KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023
[Inatolewa Chini ya Kanuni ya 118(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020] DODOMA 6 Mei, 2022
Upatikanaji wa umeme Viwandani;
Kamati ilitembelea viwanda viwili na moja ya changamoto iliyoripotiwa ni upatikanaji wa umeme usio wa uhakika; Katika kiwanda kimoja ndani ya masaa manne umeme ulikatika zaidi ya mara kumi; Ni Rai ya Kamati kwa Serikali, kuongeza kasi katika miradi ya uzalishaji wa umeme ili sasa umeme uweze kuwa wa kutosha kuhudumia maeneo mengi.
Aidha, kwa maeneo ya viwandani, Serikali iweke msukumo katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme ni wa uhakika, vilevile, kuwepo na laini ya umeme wa viwandani ambayo ni tofauti na laini ya majumbani ili sasa hata kama umeme unakatika kutokana na hitilafu ndogondogo basi zithiathiri upatikanaji wa umeme wa viwandani.
SOURCE: SEHEMU YA TAARIFA YA KAMATI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA (FUNGU 44) KWA MWAKA 2021/2022 PAMOJA NA MAONI YA KAMATI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FUNGU 44 KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023
…………………………………........
TAARIFA YA MWAKA YA SHUGHULI ZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI KWA KIPINDI CHA JANUARI, 2021 HADI FEBRUARI, 2022
[Imetolewa chini ya Kanuni ya 136 (15) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020]
Mheshimiwa Spika, Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ni mradi muhimu sana hasa ikizingatiwa kuwa ni Mradi wa Kimkakati. Ni matamanio ya Kamati kuona kuwa Mradi huu unakamilika kwa wakati ili kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.
Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, Kamati hairidhishwi na kasi ya utekelezaji wa mradi huu kwani maeneo mengi yapo chini ya wastani wa utekelezaji kimkataba.
Mheshimiwa Spika, Kamati inasikitishwa na sababu zilizotolewa kuhusu kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini kwani Kamati inaona kuwa kukatika umeme mara kwa mara ni jambo ambalo lingeweza kuzuilika endapo Serikali ingechukua hatua madhubuti kwa kutekeleza mpango wa ukarabati wa miundombinu ya TANESCO na kuipatia fedha za kutosha kwa ajili ya ukarabati.
SOURCE: SEHEMU YA TAARIFA YA MWAKA YA SHUGHULI ZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI KWA KIPINDI CHA JANUARI, 2021 HADI FEBRUARI, 2022
Kwa kuwa maneno hayo ya dhihaka kwa Bunge yametolewa na Waziri Makamba sasa kuna ulazima Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson pamoja na Wenyeviti wa Kamati hizo mbili kutoa tamko kuhusiana na Kamati zao kushushiwa heshima mbele ya umma ili hali kamati hizo zinatuwakilisha sisi wananchi.