Uchaguzi 2020 Bunge lijalo litavunja rekodi ya kupitisha hoja kwa haraka sana

Uchaguzi 2020 Bunge lijalo litavunja rekodi ya kupitisha hoja kwa haraka sana

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
567
Reaction score
1,564
Kama wewe ni Mpenzi wa kufuatilia Vipindi vya Bunge basi Malizia Hamu yako kwa kusikiliza Bunge Hili la Sasa.

Nasema hivi kutokana na Ukweli kwamba sioni dalili njema kwa Wapinzani kupita katika nafasi za Ubunge katika Uchaguzi ujao. Naona kama kuna kila Namna, Mbinu Chafu, Hujuma na pia kutumika Kwa Mabavu ili kuhakikisha Upinzani hawapati nafasi za Wabunge kushinda katika Uchaguzi ujao.

Likiwezekana hili basi Bunge lijalo litakua linatumia Muda Mfupi sana kujadili na kupitisha na kuunga Hoja watakayoletewa mbele yao. Hii itatokana na kwamba Wabunge Wadadavuzi,waibua Hoja, na Wabeba maono hawatakuwepo.

Hivyo wewe kama ni Mpenzi wa Bunge la Hoja fuatilia hili la sasa hivi ndio la mwishomwisho.

Bunge lijalo Hoja zitaungwa Mkono hata kabla Hazijaletwa Mezani
 
Hakutakuwa na bunge. Itakuwa formality tu kuita bunge lakini kiuhalisia kutakuwa na kikundi kinachoitwa Rubber Stamp Parliament.
 
Uchaguzi kama utafanyika na serikali kupitia tume wakaamua kutumia mabavu basi ndio kwaheri Tanzania, mwenye masikio na asikie.
 
Back
Top Bottom