Bunge lijifunze kwa ongezeko la tozo za miamala ya simu

Bunge lijifunze kwa ongezeko la tozo za miamala ya simu

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Kwa mtazamo wangu kuna kitu muhimu Bunge linatakiwa kujifunza hapa

1. Pale wanapo ambiwa kwa maneno matamu kuwa bei itaongezwa kidogo tu, waombe kabisa hiyo draft ya ongezeko ili wajiridhishe kuwa wanachoambiwa ndio kitakachowafikia wananchi; tofauti na hapo inakuwa haileti picha nzuri kwani naamini kabisa wabunge wetu walipitisha sheria bila kujua kuwa bei ya miamala ingekuwa kubwa kiasi hicho

2. Na hii iwe kwa kila bei inayo pendekezwakuongezwa, mfano wakiambiwa bei itaongezeka shs 200, hata kama kuna kodi nyingine (VAT) juu ya hiyo 200 waambiwe pia ili itakapokuwa kwenye utekelezaji waweze kutetea serikali; Mfano unaweza kuambiwa Petrol imeongezwa shs 100, wakati wa utekelezaji ukakuta labda imeongezwa shs125 nk

Huo ni mtazamo wangu na hisi unaweza kuwasaidia wawakilishi wetu
 
Bunge hili linaloongozwa na hawa wabugia mbaazi linawezaje kuwa na product yoyote ya maana, hawa wanapigapiga meza tu ili wapate posho yakununulia mbaazi zao basi, kwakweli tumepatikana sana watanzania
 
Pamoja na hayo maelezo,wanapitisha tozo wameongea saa ngapi na lini na wananchi wanaowawakilisha?Ndo mafiga3
 
Tusitegemee chochote cha maana toka kwa hawa wademkaji.
 
Hilo genge ni mzigo kazi yao kudemka tu, ni genge la wahuni hatuna bunge TZ.
 
Hatuna Bunge kabisa.
Yaani wamekaa miezi karibia 4 wamepitisha mavitu ya kijinga halafu wanakuja na maigizo eti wamekosea.
Nashauri wajiuzulu au warudishe posho zote walizolipwa kupitisha huu upuuzi wao.
 
Back
Top Bottom