MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,011
- 2,185
Thrd hizi tunajaribu kudadavua kwa nini Silaa alisema Wabunge hawalipi kodi. Ofisi ya Bunge inasema Wabunge wanalipa kodi, ikimaanisha PAYE. Upande wa pili, Spika akitumia nguvu nyingi sana kumtia adabu Silaa kwa matamshi yake.
Nionavyo, ni kweli Wabunge wakisaidiwa na ofisi ya Bunge, wanakwepa kodi. Wanatumia mtindo wa kizamani, wa kifisadi kukwepa kodi. Mshahara wa Mbunge milioni 2 plus, marupurupu ni zaidi ya milioni 8! Jumla yote milioni 11!
Unawezaje kulipa kodi ya milioni 2 kama PAYE wakati kipato chako ni milioni 11? Nchi gani dunia hii inayolipa marupurupu mara 4 zaidi ya mshahara wa mtu?
Hii ni mbinu inayofanywa na ofisi ya Bunge ili kuwasaidia wabunge kukwepa kodi. Wabunge lipeni kodi stahili, Silaa yuko sahihi!