Bunge lipitie kanuni ili kuunga hoja mkono iwe kwa Kusimama na wale wasiokubaliana na mchango au majibu wawe wanakaa

Bunge lipitie kanuni ili kuunga hoja mkono iwe kwa Kusimama na wale wasiokubaliana na mchango au majibu wawe wanakaa

Tardy

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
1,287
Reaction score
1,607
Imekuwa ni desturi kwa Bunge letu Tukufu kupongeza,kushangili,kuzomea ,kupiga magoti,kupiga sarakasi nk.

Utukufu wa hili jumba unauhalisia kwa Mungu na wananchi?

Mbunge akichangia iwe kwakumdhihaki Waziri, Makofi hupigwa.

Waziri akimjibu muuliza swali anajibu kwa dhihaka akikebehi nchi jirani,Makofi hupigwa.

Spika akitolea ufafanuzi Makofi hupigwa.

Bunge limekuwa linatumia mda mwingi kushangilia hali inayoleta kelele tu Bungeni hadi Spika anachukua mda mrefu kuwatuliza huku wabunge hawaeleweki wanasimamia nini.

Bunge lipitie kanuni yakushangilia kwa kupiga Makofi kuunga hoja kwa Kusimama na wale wasiokubaliana na mchango au majibu wawe wanakaa.

HESHIMA BUNGENI NDIO HESHIMA YA TAIFA LETU.
 
Waache jaman wamepambana kuingia pale

Wewe pambana na jipambanue na gharama za maisha zinazopanda
 
Waache jaman wamepambana kuingia pale

Wewe pambana na jipambanue na gharama za maisha zinazopanda
Gharama hazianzishwi huku chini,zinaanzishwa juu wanakoturatibia Nchi iweje.Huwezi kupambana peke yako kama mtoto bila mzazi huku anaboronga.
 
Back
Top Bottom