Ndugu,
Binafsi nimekuwa na mashaka na integrity ya uteuzi wa Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba.
Mashaka yangu yanarokana na kauli alizotoa Rais Kikwete - Mbeya Jumapili iliyopita na Dar es Salaam jana kwenye mkutano wa Baraza la Vyama Siasa kuwa amekuwa akitumiwa vi-memo akiombwa kuwateua akina fulani.
Ni vigumu kuamini kuwa Ikulu imepoteza integrity kiasi hicho! Aidha ni vigumu kuamini kuwa watu walioteuliwa kwa vi-memo wanaweza kuwakilisha maslahi ya umma badala ya masuala yao binafsi, hata kununuliwa na vikindi maslahi.
Nina mashaka iwapo Bunge Maalum la Katiba halitakuwa limejaa mabarakara.
Tumeliwa!