Naona Bungeni kwachafuka. Baada ya Mhe. Jaji Warioba kupewa nafasi ya kwasilisha Rasimu ya Katiba Wahe. Wabunge wameendelea kupiga kelele, kugonga gonga meza na hivyo kukawa hakuna amani na baadaye kikao cha Bunge kikaahairishwa na Mhe. Spika. Kwa kweli siyo jambo la kiungwana kwa Wahe. Wabunge kufanya vitendo visivyo na maadili mbele ya Watanzania.