Bunge Maalum linapogeuzwa 'Lecture Room'

Bunge Maalum linapogeuzwa 'Lecture Room'

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Ninaamini kuwa Wajmbe wote wa Bunge Maalum la Katiba ni watu makini. Ni watu wenye sifa mbalimbali za elimu,ujuzi na fani.Wanazo sifa za kuwafanya kuwepo Dodoma Bungeni. Kila Mjumbe anajua kilichompeleka Dodoma, yaani,kujadili na kupitisha Rasimu ya Katiba.

Ninaamini pia kuwa kulikuwa na ulazima wa kuwapa semina Wajumbe wa Bunge Maalum juu ya Kanuni zao wakati zilipokuwa zikiundwa.Mantiki hapa ni kuwa Kanuni hizo hazikuwepo kabla. Vyema walivyojadili na kukubaliana juu ya Kanuni zao achilia mbali Kanuni za 37 na 38 zilizobuma.Kanuni hizi zinajikita kwenye namna ya kufanya uamuzi Bungeni na kama itumike kura ya wazi au ya siri.

Lakini,siamini kama kuna ulazima wa kuwahutubia Wajumbe juu ya Muungano. Kila Mjumbe Bungeni humo ni mtanzania.Anajua,kama si kupitia shuleni basi mtaani,kuhusu Muungano. Na isitoshe,Jaji Warioba atawafafanulia vyema kuhusu Muungano na kujenga hoja za kwanini kuwe na aina ya Muungano wa Serikali tatu.Wasikilize kwa Jaji Warioba na waanze kujenga cha kujadili.

Nasema,hakuna haja ya wanaoitwa 'Wanaoujua Muungano' kwenda Bungeni na kutoa mhadhara juu ya Muungano. Itakuwa ni kupoteza muda na rasilimali nyinginezo. Itakuwa ni kufanya mashindano ya nani ni Mwalimu mzuri kwa Wajumbe na hiyo haitasaidia kitu.Na wala si suala lililowapeleka Dodoma.

Ni wazi kuwa kila Mjumbe anapaswa awe tayari au anaelekea kujisomea nyaraka mbalimbali zinazoweza kumsaidia kujenga hoja jadilifu wakati wa kujadili Rasimu ya Warioba. Hakuna haja ya kuwaleta 'Malecturer' wa Muungano katika muda huu.Muungano unajulikana. Sasa ni muda wa kujadili,kwa sababu zenye maana, aina ya muungano tuutakao. Hakuna haja ya mihadhara ya Mapuri,Ngwilizi,Kavishe au yeyote awaye juu ya Muungano.

Bunge Maalum lisigeuzwe 'Lecture Room'. Muda unakwenda na rasilimali zinazidi kuteketea.Si jambo jema hata kidogo
 
Back
Top Bottom