Bunge na Watanzania kwa ujumla, tulichukua hatua gani kwa waliohusika na madudu katika Ripoti Ya CAG iliopita? Another political silly season!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Binafsi sishangai haya yaliobainishwa katika Ripoti ya CAG ya 2021/2022, bali nawashangaa wanaoshangaa yaliyoibuliwa katika ripoti hii.

Kama `Bunge lenye wajibu wa kuisimamia serikali halikuchukua hatua kuhakikisha waliousika na ubadhirifu na ufisadi katika ripoti iliyopita wanachakuliwa hatua huku watanzania tukiendelea na hamsini zetu kama hakuna kilichotoea zaidi ya kelele za mitandaoni, leo mnashangaa nini katika hii ripoti ya 2021/2022?

Kwa maneno mengine, Watanzani tulitarajia nini cha tofauti safari hii?

Kelele zetu na za wenye mamlaka kuhusu hizi ripoti ni sawa na maji ya moto, hivyo tuache wajanja wajipigie.

Tuache unafiki.

New political silly season begins in our beatiful country.
 
Huu mjadala wa report ya CAG wenyewe haudumu hata siku mbili.

Kamala yupo na waandishi wa habari wa kimagharibi wanauliza maswali ya ushoga tu.

Mama yenu atajichanganya kujibu ndiyo inakuwa topic mpya!
 
Mama naye anazuga tu.
 
BUNGE hili hili la MAKADA WATUPU kwani REPORT ya Mwaka jana ulisikia BUNGE LILIAGIZA NINI KWA SERIKALI DHIDI YA MAFISADI?
 
Binafsi sishangai haya yaliobainishwa katika Ripoti ya CAG ya 2021/2022, bali nawashangaa wanaoshangaa yaliyoibuliwa katika ripoti hii.

Kama `Bunge lenye wajibu wa kuisimamia serikali halikuchukua hatua kuhakikisha waliousika na ubadhirifu na ufisadi katika ripoti iliyopita wanachakuliwa hatua huku watanzania tukiendelea na hamsini zetu kama hakuna kilichotoea zaidi ya kelele za mitandaoni, leo mnashangaa nini katika hii ripoti ya 2021/2022?

Kwa maneno mengine, Watanzani tulitarajia nini cha tofauti safari hii?

Kelele zetu na za wenye mamlaka kuhusu hizi ripoti ni sawa na maji ya moto, hivyo tuache wajanja wajipigie.

Tuache unafiki.

New political silly season begins in our beatiful country.

Hiyo ripoti ya CAG imekuwa ni kama hadithi za magazeti ya udaku tu. Kama kila mwaka uchafu unasomwa na hakuna hatua zozote zinachukuliwa, nitashangaa sana watakaokuwa na nafasi huko serikalini waache kuiba hizo pesa. Walioko kwenye ulaji waendelee kula hadi hawa wananchi Mazezeta watakapoamka.
 
Ameshaona sisi ni mazoba, kaona bora anunue magoli tu huko kwenye mpira.
Wanajuana ndio maana hawachukuliana hatua(ukoo wa panya).

Amejua akili zetu ziko kwenye mpira, kaamua kutupa tunachopenda.
 
Back
Top Bottom