Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BUNGE: THE THEATRE OF VERY RARE TALENTS
Uwanja wa Manchester United jina lake halisi ni Old Trafford lakini wenyewe mashabiki wa timu hiyo wanauita uwanja wao, "Theatre of Dreams," yaani Jumba la Ndoto.
Wapinzani wao wakubwa Liverpool vijana wa Merseyside washabiki hubeba mabango wakiwa ndani ya Old Trafford siku wanacheza na Man U yaliyoandikwa, "Theatre of Nightmares!"
Ujumbe uliokusudiwa ni kuwa leo hapa Man U hamlali mkaota njozi nzuri hapa leo ni jinamizi mwanzo mwisho.
Bunge letu lina mengi ya kustarehesha katika ubingwa wake wa sanaa za maonyesho ya uchekeshaji na kwa kweli baadhi ya wabunge wetu ni mabingwa khasa wa kuweza kupambanishwa na Laurel Hardy na Stan Lawrence au na Charlie Chaplin au Eddie Murphy.
Hawa walikuwa wachekeshaji wakubwa sana duniani wakifahamika khasa na watoto duniani kote kwa vituko vyao.
Lakini muhimu ni kuifunza akili yako iweze ku-appreciate art bila ya hivyo unaweza kudhani kivazi chako adhim cha adabu, lebasi yako ya kwendea masjid na kwenye hafla kama harusi na mialiko mingine kinachezwa shere.
Inataka utulivu mkubwa wa akili.
Bunge letu ni, "Theatre of Very Rare Talents."
Wala si ile, ''Karagosi Kalewa Tembo,'' tuliyokuwa tukiangalia Mnazi Mmoja siku ya Eid tulipokuwa watoto.
Si kila Bunge duniani utakuta vipaji kama hivi.
Tanzania Mungu katubariki kwa mengi.