Kwa uhalisia linapokuja suala la Zanzibar, Wazanzibar wote huwa wamoja, hakuna cha CUF wala CCM. Wote wanatetea maslahi ya nchi yao.. Sisi huku bara Wabunge wa CCM ndiyo maadui wetu, badala wasimame kidete kutetea maslahi ya Tanganyika wao wamekaa kulinda maslahi ya CCM...
Lakini hebu wajiulize si CCM hata wale wenye kutetea serikali mbili,, ni nani yupo nyuma ya kuhakikisha Serikali tatu hazipiti ili tuendelee na Serikali mbili wakati taasisi nyeti kama Baraza la Wawakilishi, Bunge la Tanzania na Ofisi ya Waziri Mkuu walipendekeza Serikali Tatu..
Kuna watu wanatumika bila kujua wanatetea kwa maslahi ya nani.. Wanaotaka kuendelea na Serikali mbili ni watu wachache wenye kutaka kuendelea kuifisidi nchi hii wao pamoja na watoto wao.
Kwa darasa alilolitoa Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba, sioni mantiki ya mapendekezo ya CCM ya Serikali mbili zilizoboreshwa...
CCM wakubali tu na wajipange upya!!