beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imetaja mambo matatu yanayochangia kupanda kwa bei ya mafuta ikiwemo uwezo mdogo wa maghala ya kupokelea na kuhifadhi mafuta nchini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dustan Kitandula ameyasema hayo leo Jumanne Februari 15, 2022 wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli za Bunge kwa kipindi cha kuanzia Januari, 2022 hadi Februari 2022.
Amesema bei ya mafuta nchini imekuwa ikipanda mara kwa mara na kusababisha kuongezeka kwa bei ya bidhaa mbalimbali, hali ambayo inapelekea mfumuko wa bei na hivyo kuongeza gharama za maisha kwa wananchi.
Kitandula amesema kuongezeka kwa bei ya mafuta kunachangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo kupanda bei ya mafuta katika soko la dunia, changamoto ya miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam na uwezo mdogo wa maghala ya kupokelea na kuhifadhi mafuta nchini.
Ameshauri Serikali kuweka mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kuboresha miundombinu ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam ili iweze kukidhi mahitaji na kupunguza gharama za kuagiza mafuta nchini.
Pia ameshauri kujenga maghala makubwa ambayo yatahifadhi mafuta zaidi ya mita za ujazo million 1.25.
“Hatua hii itaifanya nchi yetu kuwa ‘hub’ ya biashara ya mafuta kwa nchi zinazotuzunguka na vilevile itawezesha nchi kuagiza mafuta mengi zaidi wakati bei ya mafuta imeshuka katika soko la dunia,” amesema.
Amesema kwa kipindi cha mpito wakati Serikali ikijapanga kujenga sehemu moja ya kupokelea shehena ya mafuta, ghala la kuhifadhi mafuta la TIPER lianze kutumika ili kuondoa tatizo la meli kusubiri kwa muda mrefu kuingia bandarini na kupunguza gharama za ucheleweshaji wa meli.
Vilevile, Kitandula amesema kamati yake imeshauri kuharakisha kukamilisha mabadiliko ya mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja kutoka zabuni ya shehena kwa shehena kwenda zabuni ya bidhaa kwa bidhaa kwa lengo la kuingiza shehena kubwa zaidi kwa kila aina ya mafuta na kupata unafuu wa gharama za uletaji wa mafuta.
“Upo ushindani usio sawa kati ya kampuni za wazawa za uagizaji wa mafuta na kampuni za nje. Kamati inaona kuwa ni muhimu TPDC (Shirika la Maendeleo la Petroli Nchini) na kampuni yake tanzu ya biashara ya mafuta iwezeshwe kimkakati ili iweze kushindana na Kampuni za nje katika uagizaji wa mafuta,” amesema.
Ameishauri Serikali ifanye mapitio ya sharia na kuja na marekebisho ya sheria yatakayowezesha kampuni zilizosajiliwa nchini kupata unafuu utakaoziwezesha kuweza kushindana na kampuni zilizosajiliwa nje ya nchi yetu.
Wameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) ikamilishe mchakato wa kutunga Kanuni zitakazowezesha uanzishaji wa vituo vya mafuta vijijini kufanyika kwa gharama inayohimilika tofauti na vituo vya mijini.
Ametaka mchakato huo ukamilike kabla ya Mei 2022 ili huduma hiyo muhimu iweze kufika maeneo mengi ya vijijini kwa urahisi.