Bungeni: Mwenyekiti PAC amtaka Kangi Lugola kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini

Bungeni: Mwenyekiti PAC amtaka Kangi Lugola kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
BAADA ya Kangi Lugola, kuwekwa chini ya ulinzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa madai ya ufisadi, sasa kuwekwa kikaangoni bungeni.

Nagenjwa Kaboyoka, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), amemtaka Lugola ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini.

Kaboyoka ametoa hoja hiyo wakati akizungumza bungeni jijini Dodoma, jana tarehe 29 Januari 2020, huku akimtuhumu Lugola kwamba alilipotosha bunge kuhusu ununuzi wa sare hizo.

“Kwa hiyo Kangi alilipotosha bunge kwa kuapa kwamba, atatoa nguo kama sare hazipo, inamaana hasomi hata taratibu,” amesema Kaboyoka.

Mwenyekiti huyo wa PAC amemkalia kooni Lugola, akimtaka aeleze sare hizo zilinunuliwa kutoa wapi pamoja na gharama zilizotumika kununua sare hizo.

“Huyo aliyepewa tenda alipatikanaje, sare zililetwa kutoka wapi, kiasi cha fedha iliyotumika ni ngapi? “ amehoji Kaboyoka.

Kaboyoka amesema Lugola akitoa maelezo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atafuatilia sakata hilo, ili kujua kama idadi ya sare aliyoitoa, inaendana na idadi halisi iliyopo.

“Kuanzia hapo ndio CAG aweze kwenda stoo kujua kuna nini kutokana na zile ripoti, aone kwamba zile sare ziliagizwa mia na zimekuja mia, kinyume na hapo CAG hawezi kutoka akaenda kwenye stoo akaangalia kitu ambacho hana nyaraka zinazoonyesha kilichomo,” amesisitiza Kaboyoka.

“Nanyanyua mikono juu itakapofika jioni kama mimi nasema uongo kwamba hakuna sare hewa, najivua nguo, kamati ya mambo ya ulinzi na usalama na maofisa ya CAG twende stoo kuu tukaangalie makontena 15 na magodauni 5 yamesheheni sare za vitambaa. Nauweka uwaziri wangu rehani kama mimi nasema uongo,” Lugola aliapa bungeni.

Lugola pia alimtuhumu Profesa Mussa Assad, aliyekuwa CAG kwamba alisema uongo katika ripoti yake, juu ya ununuzi wa sare hizo.

“CAG amelihusisha Jeshi la Polisi na kashfa ya sare hewa, na kwamba sare hizi ni za bilioni 16.6. Kwa heshima na taadhima kwa moyo mkunjufu, kwa mikono yangu meupe nikiwa kama waziri makini, ambaye naitakia mema nchi hii, natetea rasilimali za Watanzania na tumuogope Mungu, sijawahi kuona mtu muongo kama CAG,” alisisitiza Lugola.

Kwa sasa Lugola anakabiliwa na kashfa ya kuingia mkataba wa kifisadi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, ambapo anahojiwa na TAKUKURU.

Lugola anahojiwa na TAKUKURU baada ya Rais John Magufuli kuiagizataasisi hiyo kuchunguza mkataba huo, kwa ajili ya kujua wahusika ili wachukuliwe hatua.

Chanzo: Mwanahalisi
 
Kangi Lugola anashukiwa kama mwewe
SURATI ZUBAA  Ndio surati zubaa, pengine tumesomewa, Sivyo tusingebung'aa, wakat ( 640 X 640 ).jpg
 
Ukiona mtu anataka aonekane ni zaidi ya wote, halafu anaweka na mbwembwe nyingi kuonekana zaidi ya wengine, weka alama ya kuuliza.

Ile kuweka viraka vya bendera ya Taifa mpaka kwenye mashati, kama vile yeye ni mtanzania kuliko wengine. Kutembea ameshikilia ilani ya CCM kama vile yeye ni mwanaCCM kuwazidi wengine, ni dalili ya uovu anaotaka kuuficha kwa mbwembwe nyepesi nyepesi.

Mwigulu naye kuvaa skafu ya bendera ya Taifa kama vile yeye ni mtanzania zaidi kuliko wengine, ni jambo kujiuliza.

Mwalimu hakuwahi hata kuvaa kofia yenye bendera ya Taifa - ina maana akina Lugola na Mwigulu wamemzidi utaifa hata Baba yetu wa Taifa!!!
 
Ninja Kange kashafanywa Mbuzi wa kafara.
Kuna mtu hapa anasema Kange anapesa ndefu kabla hata ya kuwa Waziri.
Wazee wa Mwibara ongezeni nyama kwenye hilo
 
Kama Lugola kapiga kwenye sare za jeshi wacha apige tu maana huu ni ujinga. Nchi huru ya miaka 60 inaagiza sare za jeshi lake nje ya nchi kama huu si uwendawazimu ni nini?.

Yaani at the expense ya jeshi letu, tunatengenezea nchi nyingine ajira badala ya kuzitengenezea humuhumu nchini ili zitoe ajira kwa watu wetu!


Uko nje ya Mada!
 
Back
Top Bottom