Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BURIANI MWALIMU AHMED RAJAB ULITOSOMESHA WENGI VIJANA KWA KALAMU NA SAUTI
Naanzia wapi kumueleza Ahmed Rajab?
Najiuliza.
Nianze nyumbani kwa rafiki na ndugu yangu Ahmed Maulid Mwanadiplomasia na Mtaalamu wa Kifaransa nilipomjulia Ahmed Rajab au nianze Heathrow London siku Ahmed Rajab alipokuja kunipokea?
Au nianze BBC aliponichukua na kunijulisha kwa watangazaji nguli wa Idhaa ya Kiswahili BBC, Bush House?
Au nianzie tukiwa tunatembea kwa miguu tukitokea kwenye treni za chini ya ardhi stesheni ya Charring Cross tunaelekea BBC Holborn?
Nianzie wapi mimi kumueleza kaka na mwalimu wangu Ahmed Rajab?
Nianzie kwenye ofisi za Africa Events au kwenye ofisi yake ya Africa Analysis iliyokuwa Barbican?
Miaka mingi sana imepita toka siku ya kwanza tuonane nyumbani kwa kwa Ahmed Maulid Masaki sote tulipoalikwa kwa chakula cha usiku.
Ahmed alikuja na rafiki yake, sasa marehemu Ali Said.
Ali Said tukijuana kabla na alikuwa akiishi Masaki kama mimi.
Kabla sijasonga mbele nataka msomaji wangu nikudokeze kuhusu hawa watu watatu niliowataja hapo juu.
Hapana hawa siyo, ‘’The Three Musketeers,’’ katika kitabu cha Alexander Dumas.
Hawa miaka ile walikuwa vijana wa Kizanzibari waliokuwa wanaijua dunia na hadhi na heshima ya nchi yao Zanzibar.
Nilikuwa kila nikizungumzanao mimi nakuwa darasani nasomeshwa.
Nilimjua Ahmed Rajab hapo nyumbani kwa Ahmed Maulid lakini nilikuwa nikimsoma sana katika Africa Events na Africa Now majarida yaliyokuwa yakichapwa London.
Makala za Ahmed Rajab zilituvutia vijana wengi wa wakati ule hasa baadhi yetu tuliokuwa tunaanza uandishi.
Ahmed Rajab alikuwa mwalimu wetu wa masafa marefu.
Mwaka wa 1991 nilikuwa na safari ya likizo nakwenda Glasgow, Scotland kumtembelea kaka yangu Prof. Mgone.
Yeye akisomesha University of Glasgow.
Nikamwambia rafiki yangu Ahmed Maulid kuwa nakwenda Uingereza na ningependa siku kama mbili tatu nikae London kisha niendelee na safari yangu kwenda Glasgow kwa kaka yangu lakini tatizo sina mwenyeji London nami ni mshamba sijafika Ulaya.
‘’Ahmed atakupokea nitamtaarifu.’’
Ahmed Maulid huyo.
‘’Hakuna shida atakupokea.’’
Sikuwa namjua Ahmed Rajab kwa kiasi hicho.
Nimemuona kwa muda mfupi nyumbani kwa somo yake Ahmed mwenzie na kidogo nikawa na wasiwasi.
Nimefika Heathrow watu wa Immigration wakanizuia kuingia tatizo lilikuwa pasi yangu imeingia nchi nyingi wanataka maelezo kote huko nakwenda kufanya nini?
Wametaka pia kujua nimekuja na fedha kiasi gani?
Fedha zangu mfukoni zilikuwa kidogo.
Vipi nitajikimu? Wanataka maelezo ya kueleweka.
Fedha nilikuwa nazo ndani ya Uingereza lakini kwa hali ya nyakati zile naogopa kueleza kuwa nina fedha Uingereza.
Huu ulikuwa wakati wa utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Dola moja kuwanayo inaweza kukusababishia matatizo makubwa.
Ahmed Rajab kasubiri hadi abiria wa mwisho katoka.
Hajaniona.
Kawaendea wasafiri wenzangu tumepanda sote ndege kutokea Cairo kama wameniona ndani ya ndege.
Wakamueleza Ahmed Rajab kuwa nimezuiwa Immigration.
Miaka ile tunaingia Uingereza bila visa sasa kipi kitawafanya Uhamiaji wanidake?
Madawa ya kulevya. Hili ndilo jibu la haraka.
Mara Ahmed Rajab anasikia jina lake linatajwa kwenye kipaza sauti anataarifiwa kuwa mgeni wake aliyekuja kumpokea atatoka punde asubiri.
Baada ya kusalimiana Ahmed akaniuliza, ‘’Kulikoni Mohamed mbona umetutia wasiwasi?’’
Rafiki yangu Mohamed Maharage Juma na yeye alikuwa kaja Heathrow kunipokea.
Wakati ule bado alikuwa hajawa Balozi.
Nikawaeleza kuwa walidhani mimi ‘’Mzungu wa Unga’’ na wanasema nilionyesha dalili hizo kwa kusema kuwa nimekuja Uingereza likizo na walipopekua mzigo wangu wakakuta navaa nguo nzuri nzuri za mitindo na vitu vingine vinavyogharimu fedha nyingi.
Fikra waliyokuwanayo Waingereza kuhusu sisi ni kuwa tulikuwa watu wa dhiki kubwa.
Lakini kilichoniokoa ni pale waliposoma shajara yangu.
Waliyosoma yaliwashangaza.
Wakataka kujua kiwango cha elimu yangu.
Hapo ndipo wakaamini kuwa nchi zote zile nilizokuwa nimeingia na kutoka nilifika kwa ajili ya kazi.
Ahmed Rajab akanipangia nyumba Finsbury Park na kunilipia, jirani ya klabu ya mpira ya Arsenal na siku hiyo usiku alipokuwa ananipeleka kupumzika tulikuta vurugu kubwa mtaani kwa sababu Arsenal ilikuwa imeshinda kikombe.
Ahmed Rajab akanikirimu mwisho wa kunikirimu akanijulisha kwa watangazaji wa BBC na watu wengi maarufu katika duru za Watanzania hasa jamii ya Kizanzibari London: Abdulrahman Babu, Mohamed Abubakar, Aisha Yahya, Mohamed Mlamali Adam, Chama Omari Matata, Ali Saleh, Ali Attas, Ali Adnan (huyu siku zote akinyoa kipara), Suluma Kassim kwa kuwataja wachache.
Ahmed Rajab akanichukua kwenye Uradi maarufu uliokuwa ukisomwa nyumbani kwa Msomi Bingwa na Sheikh Mohamed Abubakar.
Ahmed Rajab akanipeleka kwingi kwenye ofisi za majarida maarufu ya London yanayoandika habari za Afrika na kunikutanisha na waandishi wake.
Halikadhalika akiniingiza katika mikutano mingi ambayo yeye alialikwa na akinijulisha kama mwandishi kutoka Tanzania.
Katika hawa namkumbuka Anver Versi wa New African ambae alikuja kuchapa makala zangu nyingi na katika hizo moja ilipata kuwa ‘’Makala ya Mwezi’’makala maalum iliyochapwa na picha ya mwandishi na kupewa kifuta jasho.
Ahmed Rajab akanifikisha hadi kwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Mzee Nelville Halmes (sina hakika ya ‘’spelling’’ ya jina lake) akanifanyia mahojiano ya kazi.
Hiki ni kisa kirefu.
Hakika sikujua kama nilikuwa katika kutihaniwa.
Hadi leo nina picha niko ndani ya studio za BBC Glasgow, Scotland nasoma kipindi nilichoandika mwenyewe, ‘’Barua Kutoka Glasgow.’’
Kipindi hiki nilikuwa naeleza kijiji cha Blantyre Scotland ambacho kiligeuzwa kuwa Makumbusho ya David Livingstone.
Blantyre ndiko alikozaliwa Dr. David Livingstone.
Kote tunakata mitaa ya London kwa miguu au ndani ya treni Ahmed Rajab ananisomesha mambo sikupata kuyajua kamwe.
Ilikuwa tukiwa ofisini kwake Barbican kwenye ofisi za Africa Analysis ndipo hapo mimi nilipokuwa napata darsa kubwa.
Huwezi kuchoka kumsikiliza Ahmed Rajab.
Ilikuwa katika ofisi hii siku aliponipa kazi ya kuandika kuhusu, ‘’Ukimwi na Ukame Afrika,’’ kwa ajili ya gazeti moja ndipo baada ya kusoma makala ile akaniambia kuwa nilikuwa na kipaji kikubwa cha uandishi na yeye angeweza kunipatia kazi katika gazeti lolote pale London.
‘’Lakini Mohamed lazima ujifunze kutumia computer huku watu hawaandiki kwa kalamu.’’
Wakati huo nilikuwa siijui computer.
Yapo mengi.
Mara ya mwisho kukutana na Ahmed Rajab ilikuwa Zanzibar mwaka wa 2023 katika uzinduzi wa kitabu cha Khamis Abdulla Ameir ambacho yeye aliandika dibaji na mimi ndiye nilikipitia mtandaoni na hadharani Zanzibar.
Mimi na mwalimu wangu sote tukakizungumza kitabu hiki: ‘’Maisha Yangu Miaka Minane Ndani ya Baraza la Mapinduzi Khaini au Mhanga wa Mapinduzi?’’
Ahmed Rajab Allah atamlipa kwa wema wake na roho safi isiyokuwa na khiyana.
Hata bila ya kumuomba alikuwa akijua tu kuwa mimi nimepewa kazi ya kukipitia kitabu fulani kuhusu Zanzibar basi ataniandikia au kunipigia simu kunifundisha kuhusu mwandishi mwenyewe ni nani, yukoje na atanieleza yale ambayo nisingeweza kuyapata kokote.
Mara kwa mara nilikuwa kila akinipigia simu nitamuuliza kuhusu kitabu alichokuwa akiandika cha maisha ya Abdallah Kassim Hanga.
Yapo mengi ambayo ni vigumu kuyaeleza yote hapa.
Kasema msemaji, ‘’Ahmed Rajab kaondoka na kalamu yake."
Mwenyezi Mungu ampokee ndugu yetu amsamehe na amtie Firdaus.
Amin.