KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 92
kichuguu,
wewe binafsi unaamini uchawi upo au haupo ? ( simaanishi kama unatumia ila nataka tu kujua kama unadhani upo na unafanya kazi au la )
Kuna haja sana ya kuwa makini hasa inapotokea kifo kama hiki; wananchi kuelezwa kuwa Marehemu alikufariki kwa uchawi...iko siku jamii itaanza kuonyeshana vidole kumtafuta mchawi ni nani miongoni mwetu; tukajikuta tunachinjana wenyewe kwa wenyewe. Ni tahadhari tu.
Kuna haja sana ya kuwa makini hasa inapotokea kifo kama hiki; wananchi kuelezwa kuwa Marehemu alikufariki kwa uchawi...iko siku jamii itaanza kuonyeshana vidole kumtafuta mchawi ni nani miongoni mwetu; tukajikuta tunachinjana wenyewe kwa wenyewe. Ni tahadhari tu.
KadaM
Naheshimu hili swali umelielekeza kwa Mhe Kichuguu...lakini nalifananisha na lile la kujiuliza Mungu yupo au Hayupo? Nadhani yote ni jinsi unavyoamini wewe na nafsi yako...sio black & white.
kuna mtu kasema science na uchawi sijui nini na nini, sasa nauliza swali: which came first, uchawi au sayansi ?" ona hapo watu watakapoteleza, mie siendelei zaidi lakini naombeni mnijibu !
Dah!
Kada umenikwida shati kweli kweli mzee wangu. Nitatoa maelezo kidogo kabla ya kujibu swali lako.
Mimi niseme ukweli ni mwanasayansi; ugali wangu weote unatokana na sayansi, na naamini kabisa kuwa chembe ndogo sana ya maisha yoyote inatengezezwa kwa carbon, oxygen, nitrogen, helium,hydrogen na phosphorus. Lakini majua limitations za science kuwa huwezi kupika hizi elements kwenye maabara na kupata maisha. Kazi ya kutengeza maisha siyo kazi ya binadamu, ni kazi ya nguvu kubwa zaidi ya binadamu. Kwa hiyo ninaamini kabisa presense ya nguvu zaidi ya Sayansi ndiyo maana naamini kuwa Mungu yupo. Hata ninapokuwa nakabiliana na tatizo kubwa sana la kisayansi huwa namwomba Mungu anisaidie kunifungulia jibu la tatizo hilo kwani naamini kuwa yeye ana uwezo wa kuona nisikoweza kuona.
Chini ya imani hiyo hiyo ya kuwapo kwa Mungu na uwezo wake, ninaamini pia kuwa kuna Shetani. Sasa kati ya nguvu za kishetani ni pamoja na uchawi.
Baada ya maelezo hayo mafupi, ninakujibu kuwa mimi ninaamini kuwa uchawi upo. Watu wasiomcha Mungu ni wafuasi wa shetani na mojawapo ya zawadi zao kutoka kwa shetani ni nguvu za uchawi.
I am not sure whether you understood my previous two posts or I am missing a point in your post.