Buriani Hamisi "Super VC 10" Kibunzi

Buriani Hamisi "Super VC 10" Kibunzi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BURIANI HAMISI "SUPER VC 10" KIBUNZI

Kila nilipokutana na Hamisi Kibunzi tutazungumza mengi kuhusu mpira wa miaka iliyopita wakati Sunderland walipompa jina la "Super VC 10."

Hii ilikuwa aina ya ndege ambazo East African Airways ikitumia kwa safari za masafa marefu: Dar/Nairobi/Addis/London.

Nakumbuka siku tulipokutana katika maziko ya Athumani Kilambo.

Kilambo akipendezewa sana na wachezaji wawili Sunderland: Hamisi Kibunzi na Arthur Mambeta.

Maneno haya Kilambo ananieleza.

"Wale watoto wawili tulitaka sana waje wacheze Yanga tuongeze nguvu," Kilambo anasema, lakini hapo tunazungumza miaka mingi imepita na yeye, Kibunzi na Mambeta hawachezi tena mpira.

Wamestaafu miaka mingi na wanakimbilia utu uzima.

Kilambo anaendelea kunieleza, "Lakini mimi nilijua wale watoto hawawezi wale hata siku moja kukubali kuja Yanga, wanaipenda sana Sunderland.

Mimi simuoni Arthur Mambeta anaweka mpira kwenye goli la Sunderland kavaa jezi ya Yanga."

Kilambo akinieleza mengi kuhusu uchezaji mzuri wa Kibunzi na Mambeta.

Kilambo alikuwa siku zote akiwazungumza hawa kama watoto wadogo kwake.

Basi siku ile ya maziko ya Kilambo nikamweleza Kibunzi habari hizi.

Alishangaa sana.
Hakupata kuzisikia.

Kwa hakika kama ungewaona Kibunzi na Mambeta pale katikati Ilala Stadium ungestarehe na kuburudika na roho na nafsi yako.

Inasikitisha kuwa leo hatuna video za mechi zile.

Kibunzi alikuwa anazuia na anapeleka mpira mbele kwa mashambulizi kwa kasi ya ajabu na kwa stamina ya kustaajabisha.

Ndiyo sababu Sunderland wakamwita Super VC 10 yaani ndege kubwa.
Hamisi Kibunzi alikuwa mchezaji muungwana na mstaarabu sana.

Nadra kumuona anafanya vurugu uwanjani.
Uungwana wake utauona hata nje ya uwanja.

Siku moja nikaletewa taarifa kuwa Kibunzi kavunjika mguu.
Ilikuwa miaka ya katikati mbele 1970s na Kibunzi keshaacha mpira.

Nikauliza imekuwaje.

Nikaambiwa kuwa alikuwa amejipumzisha chini kwenye mkeka nyumbani kwao uani ukuta ukaporomoka tofali likampiga mguuni.

Siku tulipokutana nikampa pole.

"Kaka Kibunzi vibuyu vyote vile unapigana na Wajaluo wa Luo Union na Abaluya hukuvunjika mguu unakuja kuvunjika mguu uani umelala?"

Kibunzi alicheka sana.

Allah mfanyie wepesi ndugu yetu huyu msamehe madhambi yake na mtie Firdaus pamoja na waja wema.

Amin.

Picha ya pili kulia waliosimama wa tatu ni Hamisi Kibunzi na picha ya pili waliosimama wa tano kulia na kushoto Hamisi Kibunzi.

1714386427340.png

1714386507143.png

1714386574274.png
 
Shukrani sana kwa madini haya, na je ni mechi ipi ya kukata na shoka ambayo hutoisahau iliwakutanisha hao miamba wawili?
 
umesahau kueka picha mzee mohammed
 
Back
Top Bottom