Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BURIANI MOHAMED MRISHO
Kifo hakizoeleki.
Taarifa ya kifo cha Mohamed Mrisho nimekisoma kutoka ukurasa wa Vuli Yeni akiandika kutoka Johannesburg.
Sijui hata nianzie wapi.
Mohamed Mrisho alikuwa katika bendi ya The Revolutions ya vijana kutoka Tanga wengi wao kama Hemedi Chuki, Mabruki na Waziri Ali wote wametangulia mbele ya haki.
Hawa wote nimejuananao toka miaka ya 1970 na nilikuwa nikipenda sana muziki wao.
Nakumbuka wakati nasoma Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) chumbani kwangu nilikuwa na stereo system na collection kubwa ya muziki wa jazz.
Mara moja moja wakinipitia kunisalimia na tusikiliza pamoja jazz kutoka wapigaji maarufu wa nyakati zile kama Bob James, Earle Klugh, George Benson na Groover Washington.
Hivi ndivyo nilivyomfahamu Mohamed Mrisho na kwa miaka mingi tukawa marafiki tukikutana sote tunafurahi na kuzungumza mengi.
Nakikumbuka kisa kimoja.
Katika miaka ya 1980s nilikuwa nakaa Hotel 77 Arusha na The Revolutions walikuwa Resident Band wakitumbuiza pale wakati wa ''diner'' yaani chakula cha jioni.
Ikawa kila jioni wakati wa chakula cha usiku nakwenda kuwasikiliza.
Miaka ile Earle Klugh na Bob James walikuwa wametoa album yenye nyimbo zilizowapendeza wapenda jazz wengi.
Mohamed Mrisho kwenye guitar na Waziri Ali kwenye keyboard ukiwasikiliza wakipiga hizi nyimbo utasema wenyewe Earle Klugh na Bob James wako Arusha pale wanatumbuiza.
Hawa rafiki zangu walikuwa na vipaji vya ajabu sana katika upigaji wa ala zao.
Wakati wa jioni walikuwa wanafanya mazoezi.
Siku moja nikaenda kuwasikiliza.
Walipomaliza wanataka kufunga vyombo mimi nikalinyanyua guitar lake Mohamed Mrisho.
Nikaanza kupiga ''introduction'' utangulizi wa nyimbo moja maarufu na The Revolutions wakiipiga - ''Summer Time,'' tofauti mimi nilipiga ''version'' ya Sam Cooke.
Ile kupiga ''chord'' za mwanzo tu.
Wote walishtuka wakageuka kuniangalia wengine midomo wazi.
''Mohamed unajua guitar.''
Mimi nilicheka sikuwa na la kusema.
Miaka ikapita nilirudi na keyboard kutoka Uingereza nikakutana na Waziri Ali Mtaa wa Mosque.
Muda mrefu tulikuwa hatujaonana.
Katika mazungumzo nikamwambia kuwa nimenunua keybord iko nyumbani.
Haraka akaniuliza aina gani?
''Casio,'' nilimjibu.
Waziri alicheka akaniambia, ''Mohamed Casio hiyo wanapiga watoto wadogo ungenunua Roland au Yamaha.''
Ikawa zamu yangu kucheka.
Mara ya mwisho kuwasikia hawa rafiki zangu wawili wakipiga pamoja ilikuwa miaka 14 iliyopita kwenye harusi ya bint yake Yanga Bwanga, Tanga Resort.
Siku ile niliwapiga hiyo picha hapo chini.
Tunamuomba Allah awasamehe ndugu zangu hawa dhambi zao na awatie peponi: