Buriani Mzungumzaji Wangu Abuu Shariff

Buriani Mzungumzaji Wangu Abuu Shariff

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BURIANI MZUNGUMZAJI WANGU ABUU SHARIFF

Taarifa ya msiba wa Abuu (na hivi ndivyo alivyokuwa akifahamika Dar-es-Salaam) nimeipata kutoka Tanga kwa shariff mwenzake, Shariff Mohamed Yahya.

Wote walipata kucheza Young African kisha Cosmopolitan.
Mohamed Yahya akiwa mlinda mlango na Abuu mlinzi.

Pamoja na taarifa hii kaniletea na hiyo picha hapo chini mechi ya Yanga na Cosmo kushoto ni marehemu Abuu na kulia ni Abeid Maulid.

Wote wametangulia mbele ya haki.

Allah awarehemu.

Abuu alikuwa mzungumzaji wangu sana kila tunapokutana (Wanetu walisoma darasa moja shule moja Kenya na wakawa marafiki kwa kuwa ugenini).

Yanga katika mechi hii iliyochezwa Karume Stadium ilifungwa 2 - 1.

Nilipokea taarifa nyingine ya msiba huu baada ya Maghrib ikinifahamisha kuwa Abuu atasaliwa Shadhilly baada ya Isha tayari kwa safari ya kwao Bagamoyo.

Mpashaji habari wangu na mimi sote tukawa na masikitiko kuwa kwa ratiba hiyo wengi watakosa kusalia jeneza.

Isha nikapokea simu kutoka kwa mwanae Yusuf kunipa taarifa ya baba yake na kunitaarifu kuwa wako njiani wanaelekea Bagamoyo.

Iko siku In Shaa Allah nitamweleza Abuu uchezaji wake wa mpira na vipi alivyokuwa hodari wa kuwatisha "strikers" kwa staili yake ya uchezaji wa "no nonsense defender" na "hard tackling."

Kitwana Manara atakuwa shahidi yangu.

Allah amfanyie wepesi ndugu yetu, amsamehe madhambi yake na amtie Firdaus.

Amin.

PICHA: Picha ya kwanza kulia ni Abuu na kushoto ni marehemu Athumani Kilambo wakiwa kwenye khitma ya Saigon.

Picha ya pili tumepiga April mwaka huu Masjid Nur, Magomeni Mapipa mazikoni kushoto ni Yakub ''Gowon'' Mbamba, Abuu, Ishaka Marande na Mohamed Said.

1724384933587.jpeg

1724384989295.jpeg

1724385028565.jpeg
 
Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun
Mwenyeezi Mungu amsamehe makosa yake na amjaaliye katika watu watakoingia katika pepo
Ahsante Sh Mohamed kwa kutujuulisha
 
Back
Top Bottom