Buriani rafiki yangu Wendo Mwapachu

Buriani rafiki yangu Wendo Mwapachu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Buriani rafiki yangu Wendo Mwapachu!

Leo jioni katika makaburi ya Kisutu tumemzika Wendo Mwapachu.

Nimemjua Wendo kwa kujulishwa kwake na Ted kama tulivyozoea kumwita.

Ted sasa hivi Chief Edward Makwai wa Siha ndiye aliyenijulisha kwake.

Wao ni ndugu wa damu na ni siku hiyo hiyo nilimjua kaka yake Juma Mwapachu na mdogo wao wa mwisho Jabe.

Siku hiyo nilikwenda kuhudhuria birthday party ya Ted rafiki na classmate form 1 D St. Joseph's Convent School.

Ilikuwa mwaka wa 1967.

Wendo akawa rafiki yangu hadi leo tunamtia kaburini.

Kuna picha mbili za kwanza za tukio moja nimeweka hapo chini, hii picha ina umri wa nusu karne.

Katika picha hiyo waliokaa kulia ni Wendo, Esther Mzena, Stella Emmanuel aliyesimama ni Kamili Mussa kulia waliosimama ni Haitham Rashid na mimi mwandishi na nyuma yangu ni Philip sikumbuki jina lake la pili ila namkumbuka alikuwa mtoto wa mmoja wa wapigania uhuru wa Afrika Kusini akisoma Shule ya Wakimbizi Kurasini sasa (Centre for Foreign Relations).

Tulikwenda picnic Kigamboni kwenye nyumba ambayo wakati wa ukoloni magavana ndipo walipokuwa wakienda kupumzika.

Baada ya uhuru nyumba hii ikawa mahali alipotakiwa apumzike rais wa Tanganyika Julius Nyerere na familia yake.

Taarifa ni kuwa Mwalimu hakuwa mtu wa kupenda kupumzika pwani mchangani hivyo nyumba hiyo sisi tukawa na fursa ya kuitumia kila tulipotaka kwani baadhi ya watoto waliokuwa wanaishi State House walikuwa vijana wenzetu.

Picnic hii ilikuwa mwaka wa 1968.

Leo naiangalia picha hii machozi yanataka kunitoka.

Hakika tumetoka mbali.
Namtazama Wendo na sura yake jamil.

Naona ni kama jana.

Picha nyingine kundi zima ''The Scorpions,'' lime ''pose.''

Kulia waliosimama Mohamed Said, Yusuf Zialor, Kleist Sykes, Bubby Bokhari, Abdallah Tambaza.

Waliochutama kulia: Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kais.

Hii ilikuwa party ya kumuaga Liliane Abbas Sykes anakwenda shule Ufaransa mwaka wa 1968.

Lily kama tulivyopenda kumwita tulikuwa tukisoma pamoja hapo St. Joseph's Convent.

Hakika ni nusu karne lakini kila nikiipeleka akili yangu nyuma naona kama jana.

Namkumbuka Wendo kama alivyokuwa tukiwa watoto wadogo na jinsi alivyokuwa ukubwani.

Wendo alikuwa mtu wa kupendeka.

Nimeweka picha nyingine Wendo akiwa na Chief Edward Makwaia na Jenerali Ulimwengu ambae leo nyumbani kwa marehemu alimzungumza Wendo na akaeleza ule moyo wake wa huruma aliokuwanao na mkono mwepesi wa kuwasaidia wahitaji.

Picha hii nilimpiga kwenye msiba wa Kleist.
Namkumbuka Wendo Mtega Mwapachu.

Wendo alikuwa mtu mwema karim hujapata kuona.

Wendo hakuwa mzungumzaji alikuwa mtu mkimya.

Mara moja moja miaka ya nyuma mimi na yeye na jamaa tukiwa pamoja Wendo kwa kutambua mapenzi yangu kwa Prof. Ali Mazrui atanieleza jinsi alivyokuwa anaburudika na "lectures," za Mazrui wakati akisoma Makerere katika miaka ya mwanzoni 1970s.

Miaka hiyo Mazrui alikuwa akifundisha chuoni hapo.

Hapo chini ni moja kati ya kumbukumbu inayoishi moyoni kwangu ambayo Wendo ameniachia.

Mwaka wa 1991 nilikuwa naondoka Dar es Salaam kwa kipindi kirefu kidogo na safari siku ya pili.

Siku hiyo kabla ya safari wakaja vijana nyumbani kwangu wanatafuta msaada wa kujenga madrasa ya kisasa ya chekechea na kuendelea Mwananyamala A wawafundishe watoto kusoma, kuandika, hesabu na Qur' an.

Hii madrasa ilikuwa imeanzishwa na Bi. Fatuma na akisomesha mwenyewe kisha wanafunzi wake wakaichukua wakimsaidia kusomesha.

Hawa vijana ndiyo wakaja na fikra mpya ya kuiboresha madrasa yao iende na nyakati.

Hawa vijana wakaamua kuja kwangu niwatafutie mfadhili.

Mimi nikawachukua hadi kwa Wendo ofisini kwake Business Centre International (BCI).

Wendo akaniambia mimi nindelee na safari yangu na wale vijana nimwachie yeye.

Kama nilivyosema kuwa Wendo hakuwa mtu wa maneno mengi.

Tukaagana.

1992 niliporudi wale vijana wakanichukua hadi Mwananyamala A kunionyesha aliyofanya Wendo.

Nimeingizwa kwenye darasa safi la kisasa lina madawati mazuri wanasoma watoto wadogo.

Wale ndugu zangu wakaniambia kuwa fedha walizopewa na Wendo wao hawakutegemea zitakuwa nyingi kiasi kile alichowapa.

Siwezi kusema mengi kwani chuo hicho kimesomesha watoto wengi Qur'an na kinaendelea kusomesha hadi leo.

Allah mfanyie wepesi mja wako huyu, msamehe dhambi zake na mtie peponi.

Amin.





Buriani rafiki yangu Wendo Mwapachu
 
Hongera sana Kaka.. kwa kumbukumbu ulizonazo upo vizuri sana.. na unatufunza mengi.. hadi picha

Kitabu cha picha na kumbukumbu zako.. kitakuwa kizuri sanaaa.. kwa kuelezea machache kwa kila picha..

Pole kwa msiba wa rafiki yako
 
MUHIMU```
➡Kuna siku marafiki tutatengana💔 hatutaonana tena wala kuwasiliana.💌

➡Wengine umri utakuwa umeenda🕢 sana wamekuwa wazee na wengine hawatakuwepo duniani.😢😰

➡Tutakumbuka🙇 tulivyokuwa tunachat💌 tutakumbuka tulivyokuwa tunapendana ❤na kushirikiana👯 tutakumbuka tulivyokuwa vijana wenye nguvu💪 tukikimbizana💃 huku na kule lkn hatutaweza kuwa pmj tena.💔

➡Labda bado tutakuwa na picha 👤za marafik zetu tutaziangalia na kukumbuka mengi.🙇💬

➡Watoto na wajukuu zetu watatuuliza
"Ni kina nani hawa👉👭?"

➡Kwa maskitiko tutawaambia "Ni wapendwa wetu tulioshirikiana na kupendana nao" ❤❤❤💋

➡Huzuni zitatufunika maana hakutakuwa na njia ya kuonana tena zaidi ya kukumbuka enzi zetu!💏

➡Huu ni wakati wa kufurahi na marafiki 👫 💃🏃 💑 👭 na kutendeana mema ili tusije kujuta baadae.🙇

➡Huu ni wakati wa kupendana na kila aliye karibu na wewe.❤❤

➡Onyesha upendo ❤ na moyo❤ wa furaha kwa kila unaechat nae kwa sasa.💞💋

➡Tunza kumbukumbu za yale mazuri unayotendewa na marafiki zako🙆

➡Tunza picha zake kwa bidii👥👤

➡Kama unakubaliana na mimi wakumbushe marafiki zako wote kuwa upendo ❤ni kitu cha thamani sana!!❤❤❤❤

Mkumbushe kila unayechati naye kuwa hataendelea kuchat na wewe milele hivyo autumie huu wakati 🌄 vizuri. 💋

Kama na mimi ni mmojawapo nikumbushe kukuthamini na kukutendea mema 💗💋🌸❤💐💕💞💓🌹🌷💐🌺
 
Hongera sana Kaka.. kwa kumbukumbu ulizonazo upo vizuri sana.. na unatufunza mengi.. hadi picha

Kitabu cha picha na kumbukumbu zako.. kitakuwa kizuri sanaaa.. kwa kuelezea machache kwa kila picha..

Pole kwa msiba wa rafiki yako
Coco...
Ahsante sana ndugu yangu.
 
Mzee Mohamed picha hazionekani kuna shida kwangu ama ni tatizo la wote? Unatufundisha mengi, nikisoma mada zako hata kabla sijahakiki mwandishi ni nani content na uandishi najua tu ni wewe.
Baba ...
Ngoja nikuwekee link ufungue tuangalie:

 
Kel...
Kuna course nilisoma zamani sana inaitwa, "How to read difficult passages."

Moja ya kutafuta kuelewa unachosoma ni kwanza kujitathmini wewe mwenyewe baada ya kushindwa ili kujijua na kuujua uwezo wako.
Kaka mkubwa kwanza pole sana kwa kuondokewa na rafiki yako pili hili jibu lako ni la kitaalamu haswa muda uliotumia kusoma haukupotea bure.
 
Sheikh Mohammed said,..
Naomba nkushaur mwalim wangu..
Umefka wakat Utuandikie kitabu cha Maisha yako na Picha zoote za Kihistoria zako utuwekee Lkn Utupe uhusiano na wote waloipgania Nchi yetu..
Hyo ni Kumbu Kumbu Nzur kwetu..
Ahsante
 
Kaka mkubwa kwanza pole sana kwa kuondokewa na rafiki yako pili hili jibu lako ni la kitaalamu haswa muda uliotumia kusoma haukupotea bure.
Nnangale,
Mimi nimemsoma "between lines," nikamwelewa.

Kwa kawaida taazia hazijadiliwi ila unaweza kuongeza kufariji kwa kutoa pole au kusema unalojua jema la marehemu.

Tujaalie kasoma taazia hakuelewa angeliuliza kiungwana kile anachotaka kukijua.

Bahati mbaya kibri kimemtangulia tena dhidi ya wafiwa.

Nakushukuru kwa kunipa pole hilo jingine la kunipongeza.
 
Back
Top Bottom