Buriani Rais magufuli, till we meet again

Buriani Rais magufuli, till we meet again

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
207
Reaction score
677
BURIANI RAIS MAGUFULI,TILL WE MEET AGAIN.

Leo 18:30hrs 26/03/2021

Yapo maisha baada ya kifo,kuthibitisha hilo,turejee kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo,Death is not a full stop but a comma,there is life after death,Rais Magufuli umeenda kimwili tuu ila kwa kazi ulizofanya katika serikali na Chama Cha Mapinduzi,bado zinaishi na zitaendelea kuishi kati yetu,

Niweke wazi msiba wako JPM umeweka wazi kilichokuwa kinafichwa na kupigwa vita kuhusu kupendwa kwako zaidi na watu wa maisha ya hali za chini yaani Wanyonge na Walalahoi,

Nimeona body language ya kila aliyekaa barabarani kukuaga,hata wale wamama waliokuwa wanapanda ukuta kuingia uwanja wa Uhuru kuja kukuaga,niliona hata wanausalama waliokuwa wakikaa pembezoni mwa jeneza lako kila liendako pale walipokatazwa kuandamana nalo likuzungusha Jamhuri Stadium,

Nimefuatilia karibu ziara zako zote toka Mwaka 2015 kwa hakika ulikuwa unafuatilia malalamiko ya wananchi wenye shida,nilifuatilia ziara zako humuhumu mitaani,kwenye Tbc1 na hata kwenye yuuchub,kila mwenye shida nilisikia wakiita,"Baba Magufuli Raisi wangu mpendwa unanisikia sikiliza hiki kilio changu,hapa mtaani huyu anatutesa,huyu amekula hela zetu,huyu ametudhulumu kiwanja,na malalamiko ya aina hiyo niliposikia mrejesho wake niliona jambo limetatuliwa,

Kwa wewe Raisi Magufuli kulitatua hapo hapo au mhusika alikwenda mbio kulitatua awe Mkurugenzi,Mkuu wa Wilaya,Waziri au Mkuu wa Mkoa kabla wewe hujaingilia,kwa namna hiyo viongozi wa wananchi wakuu wa Mikoa na Wilaya walikuwa wapo karibu sana na wananchi kwa hofu lisije likavuja jambo akapokea simu ya kuwa huna kazi subiri utapangiwa kazi nyingine,wewe mkuu hapo tafuta mtu akamate kazi yake huyu hafai...Hilo Mheshimiwa Magufuli uliiweza kwa kutumia ile sentensi ya mwalimu Nyerere usimuonee haya mtu.

Hayati Raisi John Pombe Magufuli ulikuwa kioo cha utawala bora Tanzania,a measuring stick,kipimo cha mtawala yeyote yule hata nje ya nchi Viongozi mbalimbali walitumia style yako,na walikiri kufanya kama Magufuli afanyavyo,nimeona Kenya,nimeona Uganda,nimeona Malawi,nimeona Botswana,nimeona Ghana,nimeona Sweden.

Kwa mtazamo huo kiongozi yeyote ajaye baada yako atasoma kutoka kwako JPM na ataelewa Watanzania walipenda kitu gani na walichukizwa na jambo gani,vyombo vingi vya serikali vilikaa sawa kwa wananchi na vyombo hivyohivyo vilitumika kuikuza haki na uwazi uliongezeka na Uhuru wa kuhoji ulikuwa mkubwa hata kuvuka mipaka,

Rais Magufuli ulikuwa na roho nzuri sana lakini chama chako bado kilikuwa kimejaa walio na roho mbaya japo ni wachache na wangebadilika taratibu, Rais Magufuli uliweza kuwadhibiti mafisadi ndani ya Chama na Serikalini,Mh Rais ili lilikupaisha sana kwa kuwa ulifanya hivi kwa ajili ya mwananchi mnyonge na mlalahoi,kwa kuwa ulipenda haki ya mnyonge idumishwe,kwa kupenda kwako maendeleo na kwa kupenda kuona mwananchi wa chini hadhulumiwi ulihakikisha unawasaidia wanyonge wanaoonewa hata kwa kutoa hela zako mfukoni,uliwajengea mazingira rafiki ya kufanya kazi,si bodaboda,si mamantilie si wamachinga na wengine wengi,

Hili ndilo lilokupa uthubutu wa kupendwa huku uraiani,mambo makubwa ambayo umeyatenda kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro kwa Ujenzi wa reli ya standard gauge mambo haya yataenziwa daima na yataendelea kuwepo.Rais ajae madarakani baada yako anaweza kuyatumia hayo yakazidi kumpa respect kwa upande wake.

Nimalizie kwa kusema tulikuamini sana Rais Magufuli tulijua jambo la kipuuzi likifika kwako waliofanya upuuzi lazima wakione cha moto,na watendaji walijua Magufuli anamaanisha na hatanii ndio maana hata kama walifanya kwa uoga lakini iliwabidi wafanye kazi kwa bidii na daima kuitafuta haki ya mnyonge popote,

Mkurugenzi akisikia kuna uozo sehemu hata kama nje ya uwezo wake alijua asipofatilia yeye ndio atawajibishwa,kwa hakika ulijua kusimamia mambo na yakaenda sawa sawa na mipango na ndoto zako za kuiona Tanzania ya uchumi wa kati inakuja,uliibana system yako and so on na matokeo mazuri tumeyaona kwa idadi ya miundo mbinu uliyojenga,reli uliyojenga,Bwawa la Umeme la Julius Nyerere,kodi uliyokusanya na kuvunja rekodi ya mapato,yote ukijumlisha ukigawanya na idadi ya wananchi wa Tanzania,tunapata kipato kilichotupeleka kwenye uchumi wa kati,tunakushukuru sana JPM.

JPM umeenda kimwili tuu ila kwa kazi ulizofanya na Serikali uliyoiacha bado unaishi kati yetu,See you when you get there,till we meet again JPM.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Image 26-3-2021 at 5.11 PM.jpg
 
MKUU NJAA ITAKUUA NA TEUZI HUPATI.UMEVAA KABISA NGUO ZA MBOGA ZA MAJANI NA NAMBA YA SIMU UNAWEKA ILA UNATOKA KAPA.

WAZAZI WAKO WALIPOTEZA PESA KUSOMESHA MPUUZI KAMA WEWE
 
Back
Top Bottom