Buriani Salim "Sammy Davis" Hariz

Buriani Salim "Sammy Davis" Hariz

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BURIANI SALIM ‘’SAMMY DAVIS’’ HARIZ
Niko njiani naelekea Tanga.
Safari nimeanza alfajir sana.

Nasinzia baada ya kupita Wami.
Naizima simu yangu kuhifadhi ‘’charge.’’

NIlipofika Tanga ndipo nikaifungua na kuona msururu wa ‘’mis calls.’’

Msg zinaingia moja baada ya nyingine na ndipo nilipoona taarifa ya kifo cha Salim Hirizi kutoka kwa Hussein Shebe akiwa Zurich, Switzerland.

Jina lake khasa ni Salim Hariz.

Baba Muarabu ukoo maarufu wa Bahashwan, mama Mzaramo.

Wazaramo ikawashinda hii ‘’Hariz’’kwao ikawa ‘’Hirizi.’’

Salim akafahamika kwa jina la Salim Hirizi.

Ukoo wa Hariz maarufu Dar es Salaam na walikuwa na mnada mkubwa Mtaa wa Nyamwezi na Narung’ombe – Hariz Auction.

Mkabala na mnada huu ilikuwa nyumba ya Mzee Kassembe nje ya nyumba hii kulikuwa na mkungu mkubwa.

Mzee Kassembe alikuwa mpiga chapa ‘’typist’’ serikalini.
Hii ni miaka ya 1950 sisi watoto wadogo.

Sifa yake kubwa tulikuwa tukiambiwa ni ‘’speed’’ yake katika kupiga type.

Kasi ya vidole vyake ilikuwa kubwa sana.

Kazi muhimu za haraka alikuwa akipewa yeye.

Namkumbuka vizuri Mzee Kassembe na mwanae Richard aliyekuwa umri wangu na tulikuwa marafiki toka udogoni kwani mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed alikuwa amepanga nyumba yao nami nikienda pale mara nyingi.

Nyumba hii inanikumbusha mwendawazimu Boimanda aliyeuliwa na Manyanga kwa kumpiga kichwa pale sokoni Kariakoo.

Boimanda akipita sana hapo kwetu.

Salim Hirizi alikuwa mkubwa kwa umri kwangu lakini alikuwa umri sawa na kaka yangu Charles Mgone.

Salim Hirizi na kaka yangu walikuwa wanaogolea kutoka Banda Beach (Ferry) hadi nga’mbo Kigamboni na kurudi.

Lakini hii ilikuwa siri kubwa nyumbani hawajui mchezo huu wa hatari waliokuwa wakicheza.

Salim namkumbuka zaidi enzi za Chipukizi miaka ya mwanzoni 1960s.

Hiki kilikuwa kikundi cha vijana wa Kariakoo wake kwa waume waliokuwa wakipiga miziki ya Kizungu katika kipindi maarufu TBC kilichokuwa kikiongozwa na Raymond Chihota ambae mwenyewe alikuwa mfanyakazi wa TBC.

Ray kama alivyokuwa akijulikana alikuwa akishirikiana na vijana wengine kama Henin Seif, Salim Hirizi, Hussein Shebe, Badrin, Yusuf Ramia, Abdul Nanji, Sauda Mohamed, Mariam Zialor, Cuthbert Sabuni, Abdallah Obeid na wengineo.

Kikundi hiki kilikuwa kikipigiwa muziki na The Blue Diamonds vijana wa Kigoa.

Huyu Abdallah Obeid alikuwa ‘’drummer’’ wa kipaji cha juu kiasi alipohamia London alipiga muziki na The Hot Chocolate kundi maarufu Uingereza katika muziki wa ‘’pop’’ katika miaka ya 1970.

Wengi katika jhawa wametangulia mbele ya haki na wengine sina habari zao kwani waliondoka Tanzania mapema sana kwenda Ulaya, Marekani na Arabuni.

Katika hali hii ndipo nilipopoteana na Salim Hirizi kwa miaka mingi hadi nilipokutananae Dubai mwaka wa 1999.

Ilikuwa nimekuja Dar es Salaam kutoka Tanga kuja kupanda ndege kwenda Dubai.

Nilipita nyumbani kwa Balozi Abbas Sykes kumuaga na yeye akanipa simu ya Salim Hirizi.

Nilikuwa nakaa hoteli moja Dubai inaitwa Carlton.

Nilifika Dubai usiku na siku ya pili jioni nikampigia simu Salim Hirizi.

Akaniuliza wapi nakaa.

Nilipomtajia ninapokaa akaniambia, ‘’Mohamed shuka chini utanikuta nakusubiri kwani nyumba yangu iko nyuma ya hiyo hoteli yako.’’

Ilikuwa jioni ya kukumbuka.

Kwa miaka mingi nilikuwa sijamuona Salim wala mke wake Bi. Amina.

Tukakumbushans mengi ya Dar es Salaam ya ujana wetu katika 1960s.

Nikamuona na mtoto wao Abdallah ambae alinishangaza kwani alikuwa akizungumza Kiingereza kwa ‘’accent’’ ya London.

Mwanae hakuwa akijua kama baba yake alikuwa mwimbaji wa sifa katika ujana wake.

Akaniuliza nyimbo gani baba yake akiimba.

Jibu lake si tu lilimshangaza Abdallah bali na yeye Salim pia.

‘’Kila ninapomkumbuka baba yako nyimbo hii, ‘’Summer Time,’’ hunijia kwani iko siku usiku napita New Africa Hotel kulikuwa na bendi ya George De Souza, vijana wa Kigoa wakipiga pale.

Hapo nikamsikia na kumuona Salim anaimba ‘’Summer Time,’’ kwa ufundi mkubwa.

Hii nyimbo ilipigwa na Sam Cooke.

Miaka mingi ilikuwa imepita.

Miaka hii ikijulikana kama ‘’The Roaring 60s.’’

Salim alinipa desk top computer ambayo hakuwa akiitumia akaniambia nichukue inisaidie katika uandishi wangu.

Salim alirudi nyumbani tukawa majirani Magomeni ambako alikuwa kajenga nyumba nzuri na wote sasa wastaafu.

Siku nyingine Salim akinichukua kwenda kumjualia hali mama yake Kinondoni Block 41.

Kila siku tulikutana Fajr Masjid Nuur.

Mimi nilikuwa nimepanga nyumba ya pili kutoka nyumba yake.

Katika nyumba hii mlango wangu ulikuwa unatazamana na mlango wa nyumba ya Salim ‘’Sal Davis’’ Abdallah.

Nani asiyemjua Sal Davis?

Nimeweka picha ya Salim Hirizi kashika The Citizen ndani yake kulikuwa na makala hii: PROF. CHARLES MGONE: A GLIMPSE AT A GENIUS SCIENTIST.

Salim alipigwa na butwaa na yale aliyosoma ndani ya gazeti lile kuhusu rafiki yake wa udogoni.

‘’Mohamed Charles yuko wapi?
Miaka mingi hatujaonana.’’

Siku ilipochapwa makala hii siku hiyo Salim alikuja nyumbani kwangu.

Hawakupata kuonana kwa miaka mingi kila mtu akaenda njia yake kutafuta maisha.

Miaka ile ya 1960s ilikuwa miaka ya wazimu.

Lakini Allah katuvusha salama.

Mwenyezi Mungu msamehe dhambi zako mja wako huyu na mtie peponi.
Amin.

1729718919803.png

Salim Hirizi​
 
Napenda uandishi wako mzee wangu, unavutia na hauchoshi kusoma, msomaji anajikuta ndani ya dimbwi la nakala zako.

Apumzike kwa amani marehemu wetu.
 
BURIANI SALIM ‘’SAMMY DAVIS’’ HARIZ
Niko njiani naelekea Tanga.
Safari nimeanza alfajir sana.

Nasinzia baada ya kupita Wami.
Naizima simu yangu kuhifadhi ‘’charge.’’

NIlipofika Tanga ndipo nikaifungua na kuona msururu wa ‘’mis calls.’’

Msg zinaingia moja baada ya nyingine na ndipo nilipoona taarifa ya kifo cha Salim Hirizi kutoka kwa Hussein Shebe akiwa Zurich, Switzerland.

Jina lake khasa ni Salim Hariz.
Baba Muarabu ukoo maarufu wa Baharoun, mama Mzaramo.

Wazaramo ikawashindi hii ‘’Hariz’’kwao ikawa ‘’Hirizi.’’
Salim akafahamika kwa jina na Salim Hirizi.

Ukoo wa Hariz maarufu Dar es Salaam na walikuwa na mnada mkubwa Mtaa wa Nyamwezi na Narung’ombe – Hariz Auction.

Mkabala na mnada huu ilikuwa nyumba ya Mzee Kassembe nje ya nyumba hii kulikuwa na mkungu mkubwa.

Mzee Kassembe alikuwa mpiga chapa ‘’typist’’ serikalini.
Hii ni miaka ya 1950 sisi watoto wadogo.

Sifa yake kubwa tulikuwa tukiambiwa ni ‘’speed’’ yake katika kupiga type.
Kasi ya vidole vyake ilikuwa kubwa sana.

Kazi muhimu za haraka alikuwa akipewa yeye.

Namkumbuka vizuri Mzee Kassembe na mwanae Richard aliyekuwa umri wangu na tulikuwa marafiki toka udogoni kwani mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed alikuwa amepanga nyumba yao nami nikienda pale mara nyingi.

Nyumba hii inanikumbusha mwendawazimu Boimanda aliyeuliwa na Manyanga kwa kumpiga kichwa pale sokoni Kariakoo.

Boimanda akipita sana hapo kwetu.

Salim Hirizi alikuwa mkubwa kwa umri kwangu lakini alikuwa umri sawa na kaka yangu Charles Mgone.

Salim Hirizi na kaka yangu walikuwa wanaogolea kutoka Banda Beach (Ferry) hadi nga’mbo Kigamboni na kurudi.

Lakini hii ilikuwa siri kubwa nyumbani hawajui mchezo huu wa hatari waliokuwa wakicheza.

Salim namkumbuka zaidi enzi za Chipukizi miaka ya mwanzoni 1960s.

Hiki kilikuwa kikundi cha vijana wa Kariakoo wake kwa waume waliokuwa wakipiga miziki ya Kizungu katika kipindi maarufu TBC kilichokuwa kikiongozwa na Raymond Chihota ambae mwenyewe alikuwa mfanyakazi wa TBC.

Ray kama alivyokuwa akijulikana alikuwa akishirikiana na vijana wengine kama Henin Seif, Salim Hirizi, Hussein Shebe, Badrin, Yusuf Ramia, Abdul Nanji, Sauda Mohamed, Mariam Zialor, Cuthbert Sabuni, Abdallah Obeid na wengineo.

Kikundi hiki kilikuwa kikipigiwa muziki na The Blue Diamonds vijana wa Kigoa.

Huyu Abdallah Obeid alikuwa ‘’drummer’’ wa kipaji cha juu kiasi alipohamia London alipiga muziki na The Hot Chocolate kundi maarufu Uingereza katika muziki wa ‘’pop’’ katika miaka ya 1970.

Wengi katika jhawa wametangulia mbele ya haki na wengine sina habari zao kwani waliondoka Tanzania mapema sana kwenda Ulaya, Marekani na Arabuni.

Katika hali hii ndipo nilipopoteana na Salim Hirizi kwa miaka mingi hadi nilipokutananae Dubai mwaka wa 1999.

Ilikuwa nimekuja Dar es Salaam kutoka Tanga kuja kupanda ndege kwenda Dubai.

Nilipita nyumbani kwa Balozi Abbas Sykes kumuaga na yeye akanipa simu ya Salim Hirizi.

Nilikuwa nakaa hoteli moja Dubai inaitwa Carlton.
Nilifika Dubai usiku na siku ya pili jioni nikampigia simu Salim Hirizi.

Akaniuliza wapi nakaa.

Nilipomtajia ninapokaa akaniambia, ‘’Mohamed shuka chini utanikuta nakusubiri kwani nyumba yangu iko nyuma ya hiyo hoteli yako.’’

Ilikuwa jioni ya kukumbuka.
Kwa miaka mingi nilikuwa sijamuona Salim wala mke wake Bi. Amina.

Tukakumbushans mengi ya Dar es Salaam ya ujana wetu katika 1960s.

Nikamuona na mtoto wao Abdallah ambae alinishangaza kwani alikuwa akizungumza Kiingereza kwa ‘’accent’’ ya London.

Mwanae hakuwa akijua kama baba yake alikuwa mwimbaji wa sifa katika ujana wake.

Akaniuliza nyimbo gani baba yake akiimba.
Jibu lake si tu lilimshangaza Abdallah bali na yeye Salim pia.

‘’Kila ninapomkumbuka baba yako nyimbo hii, ‘’Summer Time,’’ hunijia kwani iko siku usiku napita New Africa Hotel kulikuwa na bendi ya George De Souza, vijana wa Kigoa wakipiga pale.

Hapo nikamsikia na kumuona Salim anaimba ‘’Summer Time,’’ kwa ufundi mkubwa.

Hii nyimbo ilipigwa na Sam Cooke.
Miaka mingi ilikuwa imepita.

Miaka hii ikijulikana kama ‘’The Roaring 60s.’’

Salim alinipa desk top computer ambayo hakuwa akiitumia akaniambia nichukue inisaidie katika uandishi wangu.

Salim alirudi nyumbani tukawa majirani Magomeni ambako alikuwa kajenga nyumba nzuri na wote sasa wastaafu.

Siku nyingine Salim akinichukua kwenda kumjualia hali mama yake Kinondoni Block 41.

Kila siku tulikutana Fajr Masjid Nuur.
Mimi nilikuwa nimepanga nyumba ya pili kutoka nyumba yake.

Katika nyumba hii mlango wangu ulikuwa unatazamana na mlango wa nyumba ya Salim ‘’Sal Davis’’ Abdallah.

Nani asiyemjua Sal Davis?

Nimeweka picha ya Salim Hirizi kashika The Citizen ndani yake kulikuwa na makala hii: PROF. CHARLES MGONE: A GLIMPSE AT A GENIUS SCIENTIST.

Salim alipigwa na butwaa na yale aliyosoma ndani ya gazeti lile kuhusu rafiki yake wa udogoni.

‘’Mohamed Charles yuko wapi?
Miaka mingi hatujaonana.’’

Siku ilipochapwa makala hii siku hiyo Salim alikuja nyumbani kwangu.

Hawakupata kuonana kwa miaka mingi kila mtu akaenda njia yake kutafuta maisha.

Miaka ile ya 1960s ilikuwa miaka ya wazimu.
Lakini Allah katuvusha salama.

Mwenyezi Mungu msamehe dhambi zako mja wako huyu na mtie peponi.
Amin.

View attachment 3133808
Salim Hirizi​
Inna li Llahi wa Inna ilayhi Rajiun.

Kariakoo tumeondokewa na kaka kipenzi.

Salim nilipomtembelea Dubai aalinipa contacts za Mwakyembe, siku hizo Mwakyembe yupo TBS na Salim ni Sales manager wa Mitsubishi Dubai.

Allah amsameh, atusameh na tuliopo njiani.

Pole sana, kwa sote, Alama.
 
Faiza,
Amin.
Sote tushapoa.
 
Poleni sana! Uzi ukiandikwa na mkongwe unakuwa na ladha tofauti sana.
 
Back
Top Bottom