Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BURIANI SHEIKH ABDALLAH MUHSIN BARWANI
Leo jioni nimepokea taarifa ya kifo cha Shekh Abdallah Muhsin Barwani aliyekuwa akiishi Dubai.
Sheikh Abdallah Muhsin ni mdogo wake Sheikh Ali Muhsin Barwani mmoja wa viongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP).
Sheikh Abdallah Muhsin amezikwa jana Jumanne tarehe 12 Julai 2022, Dubai.
Nilifahamiana na Sheikh Abdallah Muhsin niipokwenda Muscat mwaka wa 1999.
Kuanzia hapo tukawa pamoja siku zote na miaka yote.
Nakumbuka wakati ule kumbukumbu za Sheikh Ali Muhsin, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,'' zilikuwa zimeshatoka 1997 miaka miwili nyuma na nakala chache zilikuwa zimefika Zanzibar.
Kitabu kilikuwa kikisomwa kwa siri na vingi vilikuwa photocopy ya photocopy.
Hapakuwa na duka la vitabu lililokuwa na ujasiri wa kukiagiza kitabu hiki na kukiuza hadharani.
Na ikitokea kuwa nacho unakificha.
Sheikh Abdallah Muhsin katika mazungumzo yetu katika vitabu na uandishi akanifahamisha kuwa yeye alikuwa anafanya tarjuma ya Sahih Al Bukhari na alikuwa juzuu ya kwanza.
Haukupita muda mrefu nikaketewa juzuu ya kwanza kwenye maboksi nigawe vitabu hivyo bure kwa Waislam.
Furaha yangu haisemeki.
Kuwa mimi Sheikh Abdallah Muhsin ananiletea Hadith za Mtume Salla Allahu Alaihi Wa Sallam nigawe kwa hii mikono yangu.
Nikashukuru sana.
Kitabu hiki kilifika hadi nje ya mipaka ya Tanzania.
Nilikwenda Dubai mwaka wa 2016 nikamkuta Sheikh Abdallah Muhsin anaishi pale.
Katika miaka hii ya katikati alikuwa kakamilisha juzuu tatu na kila moja ikikamilika ananiletea maboksibkwa maboksi niwagawie Waislam.
Juzuu hizi za "Tarjuma ya Sahih Al Bukhari Hadithi Za Mtume Salla Allahu Alaihi Wa Sallam," zipo katika Maktaba yangu.
Ziangalie kwenye picha ya mwisho hapo chini.
Picha ya kwanza wa kwanza kulia ni Sheikh Abdallah Muhsin, Sheikh Ali Muhsin, Mwandishi na Farouk Abdulla Muscat 1999.
Picha ya pili kulia ni Sheikh Muttalib, Mwandishi, Said Baalawy, Dr. Gharib na Sheikh Abdallah Muhsin.
Tunamwomba Allah amweke mahali pema peponi.
Amin.