Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BURIANI SHEIKH AHMED HAIDAR
Sheikh Ahmed Haidar...
Mtoto wa Sheikh Haidar Mwinyimvua mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU.
Sheikh Ahmed Haidar mtu mwenye ilm kubwa sana kutoka Azhar.
Mpole, "humble," ndani ya mifupa yake.
Hata siku moja hakuonekana katika meza kuu za watu wa serikali na wanasiasa.
Hata siku moja hakuonekana ndani ya majoho ya kifahari ya kumeremeta na kanzu na kofia za kuvutia na vilemba vikubwa anaonekana akipeana mikono na wakubwa picha iko ukurasa wa mbele ya magazeti ya chama na serikali camera za televisheni zikim-zoom.
Sheikh Ahmed Haidar hakupata kutokea kwenye televisheni mimi sikumbuki.
Sheikh Ahmed Haidar hakualikwa kwenye majumba ya wafalme kwenda kunywa na kula na wala hakujisikia unyonge au kuhisi kapungukiwa kwa wenzake kualikwa huko na yeye hayumo kwenye orodha ile.
Sheikh Ahmed Haidar alitosheka na msikiti wake wa Mwinyikheri Akida.
Sheikh Ahmed Haidar mtu mkimya mpole akitembea ameinamisha kichwa chake chini anaitazama ardhi ya Allah alitosheka na nduguze Waislam na moyo wake uliridhia.
Hakuutamani ukubwa na yale yaliyowahangaisha wengi.
Mimi najifaharisha na nasema huku shingo nimetoa kuwa Sheikh Ahmed Haidar alikuwa rafiki yangu tukipata nafasi na wasaa tukizungumza na wakati mwingine akitabasamu na akicheka na mimi lau ni miaka mingi imepita nilipokuwa na fursa hii.
Sakata la Salman Rushdie mwaka wa 1989.
Sheikh Haidar kaniita baada ya sala ya Dhuhr ambayo tukisali pamoja mara nyingi nikiwa mjini.
Akaniuliza Salman Rushdie kwani kasema nini?
Nayajua yote aliyosema lakini siwezi kumwambia Sheikh.
Nani anaweza kuwa na ujasiri wa kurejea tusi aliloelekezwa Mtume SAW?
Sheikh Ahmed Haidar alim, mwanazuoni mjuzi ananiangalia anaona nakwepa kumtazama usoni naangalia chini, pembeni na kote ila uso wake.
Kila akiniuliza kitabu kinasemaje maneno yanapandana.
Sheikh akatambua nimejaa hofu na haya.
Sheikh ananijua hii si kawaida yangu naogopa.
"Usiogope nataka nijue Salman Rushdie amesema nini niambie usinifiche nieleze kila kitu nataka nijue."
Sauti ya Sheikh ilikuwa imekaza kwa msisitizo kwangu.
Nilikuwa nimeletewa "cutting," za magazeti kutoka Marekani yote yamejaa habari za "Satanic Verses," kitabu cha Salman Rushdie.
Nikaanza kumueleza Sheikh Ahmed Haidar yote niliyosoma.
Sheikh yuko kimya ananisikiliza.
Nilipomaliza Sheikh Haidar akasema, "Huyu hukumu yake ni kuuawa."
Kila Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Sheikh Ahmed Haidar alikuwa akisalisha Sala ya Tarweh Msikiti wa Kitumbini.
Baba yake alikuwa akitoka Magomeni kuja kusali Tarweh pale na akisali nyuma ya mwanae.
Naamini kwa Sheikh Haidar Mwinyimvua hii ilikuwa kipeo cha juu kabisa cha fahari kukisikia kiraa kile cha mwanae.
Na hakika ukimsikia Sheikh Ahmed Haidar anasoma Qur'an utafurahi.
Kiraa chake kilikuwa kinagonga moyo.
Sheikh Ahmed Haidar alipata kumwambia mtu kuwa anataabika sana kila anapomuona baba yake kasimama nyuma yake yeye akimsalisha.
Itapita miaka mingi sana kuja kumpata mwanazuoni kama Sheikh Ahmed Haidar.
Tunamuomba Allah amfanyie wepesi safari yake hii.
Amin.