BURIANI Sultan Jamshid BIN Abdulla BIN Khalifa (1926 - 2024)

Mzee tunaomba historia ya Tito Okello...huyu Mganda aliyekodishwa na Serikali ya Tanganyika wakati wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar
 
Stux

Stux...
Kuwinda nguruwe ilikuwa kitu cha kama burudani mfano wa watu huku kwenda porini kuwinda swala.

Linatoka kundi kubwa kuingia porini na kuanza kusaka nguruwe.
Kisha baada ya kuwinda na kukamata hao nguruwe walienda kuwaala na kuburudika kupitia nyama tamu ya nguruwe na pombe.
 
Kwa hiyo unataka kusema Kitabu cha Ghassanry ndio Ukweli pekee na Historia nyingine yoyote ni Uongo
Fainali ...
Itapendeza kama hilo aseme mtu mwingine aliyesoma kitabu hicho.

Mimi ni sehemu ya utafiti na uandishi wa kitabu hicho.
 

Sawa mtanganyika mkatoliki unayeumia zaidi kwa Zanzibar kuliko sisi wazanzibari wenyewe.

Hivi unaweza kuteletea jina la mtu mmoja tu aliyefungwa na kuuliwa na Mfalme ?? mimi nitakuletea listi ya watu waliouliwa na hao wakotiliki wenzako pamoja na Nyerere mwenyewe hapa Zanzibar na mpaka juzi bado wanaendelea kuuliwa na legacy ya kikatoliki
 
Embu tuelezee ushiriki wa Kanali Ali Mahfuodh katika Mapinduzi hayo,kwanini alikwenda Cuba kupata mafunzo makali na kukubali kuumia tena kwa hiari yake mwenyewe wakati Zanzibar kulikuwa na Raha na hakukuwa na ubaguzi au udharimu wa hao masultani?
Fainali...
Vijana wengi wa Kizanzibari walikwenda Cuba na Urusi na hawa walikuwa na siasa za mrengo wa kushoto.

Hawa walijulikana kama "Makomredi," au "Progressives," wakifuata siasa za Marx na Lenin.

Azama yao kuu ilikuwa kuifanya Zanzibar iwe nchi ya Kisoshalist.

Nchi ya Kisoshalist Usultani na aina nyingine yoyote ya utawala hauna nafasi.
 

Jemshid hakupindulia na watu wake, bali walikuwa wavamizi kutoka Tanganyika wakiongozwa na mganda
 
ye ni nani kwangu mimi mtanzania

Yeye ni mtu wa wewe kumjua ili uone Nyerere na CCM yake walivyokuwa waongo na watu wa kupiga propaganda za kuifisidi Tanganyika na Zanzibar yake
 
Msijali sahivi Zanzibar ni koloni la Tz bara tutaendelea kuwatawala kwa haki
Hakuna nchi ilyoitwa na inayoitwa Tanzania bara , kuna nchi inayoitwa Tanganyika iliyojivalisha koti la Tanzania
 

Mapinduzi ya Zanzibar hayakuwa hitaji la wazanzibari, Jaribu kusoma historia vizuri ndugu.
 
Kwa hiyo utawala wa kisultan ulikuwa hauna dhuluma, mauaji, mateso au uonevu wowote kama mzee Mohamed Said alivyosema?


cc
Proved

Utawala uliopinduliwa si wa Sultani kama CCM na Nyerere wanavyowadanganya, Iliyopinduliwa ni serikali ya Waziri mkuu Muhammed Shamte , Mpemba wa Ole. Alikamatwa na Nyerere na kufungwa zaidi ya miaka 10 jela huko Tanganyika bila ya kufikishwa mahakamani, waliofungwa ni pamoja na baraza lake la mawaziri .

Yaani Watanganyika mna damu mikononi mwenu na deni kubwa sana kwetu Wazanzibari
 
Huyu mzee unaweza kusikia anasema alikuwepo kwenye mapinduzi matukufu
Faana,
Jitulize tuwe na mjadala wa heshima sote tunufaike.

Kejeli hapa si mahala pake.

Mimi sikuwapo katika mapinduzi lakini nilikuwa katika utafiti wake.

Nimejifunza mengi.

Ninaweza nika-share niliyojifunza na ndugu zangu hapa jamvini na sote tukanufaika.
 
Huyu Mzee kila siku anamdisi Mwalimu Nyerere aliyeongoza harakati za uhuru wetu, ila huyu hapa anamsifia Sultani aliyepinduliwa kwa kuwanyima haki za kisiasa n.k wazanzibar.
Kisa na mkasa; Dini.
Utumwa wa kifikra ni mbaya sana kuliko hata kufungwa minyororo
 
Kuna sehemu ninatanzika kidogo!

Bila shaka sultani alikuwa muislamu...

Sasa iwaje awinde nguruwe? Au lengo lilikuwa ni genocide kwa nguruwe hao?
Kuna methali inasema
Ukitaka kula nguruwe chagua aliye nona

Unafikiri huu msemo wa kiswahili uliletwa na watu wa bara?
 
Niwie radhi ndugu yangu, yote niliyokukwaza nayo uyafute na kuyachukulia utani
 
Stux

Stux...
Kuwinda nguruwe ilikuwa kitu cha kama burudani mfano wa watu huku kwenda porini kuwinda swala.

Linatoka kundi kubwa kuingia porini na kuanza kusaka nguruwe.
Sasa nimeelewa kwanini waswahili walitupa methali hii:

Ukitaka kula nguruwe chagua aliye nona
 
Utumwa wa kifikra ni mbaya sana kuliko hata kufungwa minyororo

Ni kweli kwani watu wanapigwa propaganda kapinduliwa sultani wakati Sultani hakuwa mwenye madaraka Zanzibar , aliyepinduliwa ni Waziri mkuu aliyechaguliwa kwa kura chini ya Tume huru ndiye aliyepinduliwa na Nyerere mkatoliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…