Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Serikali ya Burkina Faso inayoongozwa na Kapteni Ibrahim Traore inatarajia kununua mabasi 500 kwa ajili ya kurahisisha usafiri na kuondoa adha wapatayo wanafunzi hasa waishio maeneo ya mijini.
Hayo yamesemwa wakati wa utoaji wa ripoti ya kikao cha kawaida cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika tarehe 5 Disemba 2024 na kuongozwa na Kapteni Ibrahim Traore.
Mabasi hayo yatanunuliwa kwa awamu mbili ambapo katika kila awamu takribani mabasi 250 yatanunuliwa.
Mwezi uliopita baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mji mkuu wa Ouagadougou nchini Burkina Faso waligoma kulalamikia adha ya usafiri wanayoipata kutokana na kutokuwepo kwa mabasi ya kutosha yaliyotengwa maalum kwa ajili yao.
Chanzo/ Source: Shirika la habari la Burkina Faso ( RTB)