The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Nchi zinazoongozwa na utawala wa kijeshi, ikiwemo Burkina Faso, Mali na Niger, zimejiondoa rasmi katika Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS).
Taarifa iliyotolewa na ECOWAS leo Jumatano, Januari 29, 2025, imeeleza licha ya kujiondoa kwao, imetaka mshikamano wa kikanda na kuweka milango wazi kwa ajili ya mazungumzo.
Aidha, nchi wanachama zilizobaki zinatakiwa kuendelea kuwapa raia kutoka nchi hizo tatu marupurupu ya uanachama, ikiwa ni pamoja na usafirishaji huru wa watu na bidhaa.
Mataifa hayo matatu ambayo yalikuwa miongoni mwa nchi waanzilishi wa ECOWAS, yalitangaza mwezi Januari mwaka wa 2024 kwamba yatajiondoa kwenye muungano huo.
Kulingana na kanuni za Ecowas, nchi inayotaka kujiondoa ilistahili kupeana notisi ya mwaka mmoja kabla ya kufanya hivyo rasmi.
Viongozi wa kijeshi kwenye nchi hizo waliwatuhumu wakuu wa ECOWAS kwa kutangaza vikwazo ambavyo walivitaja kama kinyume na matakwa ya raia.
Hata hivyo, Mali, Niger, na Burkina Faso waliunda muungano wao unaojulikana Alliance of Sahel States (AES), baada ya ECOWAS kushutumu mapinduzi ya kijeshi na kusimamisha ushirika wao, kwa matumaini ya kurejesha utawala wa demokrasia.
Soma: Ramani mpya ya ECOWAS baada ya Mali, Niger na Burkina faso kujitoa