Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Wanamgambo wanaosadikika wa kundi la Jihad wamevamia kijiji mashariki mwa Burkinafaso na kuua wanakijiji wanaokadiriwa 30.
‘Kundi kubwa la watu wenye silaha lilivamia kijiji cha Kodyel jimbo la Komandjari jumatatu asubuhi na kufanya shambulio liligharimu maisha ya watu wanaokadiriwa kufikia 30. Kama idadi ya vifo ipo sahihi hili linakua shambulio la hatari zaidi kuwahi kutokea nchini’alisema afisa habari.
Mashambulio ya kiislamu yameongezeka nchini hasa mikoa inayopakana na nchi za Niger na Mali. Shambulio hili linakuja wiki moja baada ya waandishi wawili wa habari raia wa Ireland waliokua sehemu ya doria dhidi ya ujangili kuuawa nchini humo.