Baha06
New Member
- Sep 16, 2021
- 1
- 0
Maisha ya amani na furaha ndiyo yenye kuleta haiba njema kwetu binadamu,na burudani ni moja ya njia ya kutupatia furaha.
Leo napenda kuzungumzia burudani nufaika kutoka katika mfano wa mchezo wa Mpira wa miguu, mchezo huu umekuwa na manufaa kwa kupitia ubunifu wa ushawishi kwa kutumia njia ya upinzani ambao umesaidia timu kupata mauzo ya hali ya juu na jamii kunufaika kutokana na shuguli za uhamasishaji wanazofanya mashabiki wa timu husika;
MFANO:
•Kwenye shughuli za kuadhimisha siku ya YANGA day na SIMBA day wote tumeshuhudia ni kwa kiasi gani watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi walihamasika na kuchangia timu zao kwa njia ya ;
Ambazo zote hizi zilisaidia timu kupata mauzo ambayo yanasaidia katika shughuli za uendeshaji wa timu.
Vilevile kama jamii kupitia maadhimisho hayo watu walinufaika kwa shughuli walizofanya kama;
Ambapo shughuli hizi ziliweza kuonekana kwa kupitia mitandao ya kijamii ambayo wamiliki wa kurasa zilizorusha matukio mbalimbali yaliyofanyika kwenye maadhimisho walipata fursa ya kuongeza idadi ya wafuasi na kufanya watambulike zaidi na kuwatengenezea nafasi nzuri kwenye ulimwengu wa kidigitali.
Licha ya yote haya bado hamasa ya kufanya burudani kuwa nufaika kwetu ni ndogo ,ni maoni yangu kuwa mashabiki wa timu za Mpira kufanya shughuli za kusaidia jamii Mara kwa Mara na wasingojee kufanya shughuli hizi wakati tuu wa kipindi cha maadhimisho.
Na ujumbe kwa timu zote za michezo nchini ni kuiga mfano uliofanywa na vilabu hivi vya YANGA na SIMBA kwa kuwaburudisha,kuwahamasisha kusaidia jamii zinazowazunguka na zenye uhitaji.

- kununua jezi
- kununua tiketi za Siku ya maadhimisho
- kupakua "APPLICATION" za timu
Ambazo zote hizi zilisaidia timu kupata mauzo ambayo yanasaidia katika shughuli za uendeshaji wa timu.
Vilevile kama jamii kupitia maadhimisho hayo watu walinufaika kwa shughuli walizofanya kama;
- kuburudika kama sehemu ya kusherehekea.
- kusaidia watu wasiojiweza ( kutoa misaada kwenye vituo vya wazee na watoto yatima).
- kusafisha maeneo ya shule ambazo zinazunguka matawi yao ya klabu za mpira.
- kutoa sadaka za shukrani kwa timu zilizofanya vizuri kwenye taasisi za dini.
- Kuwatembelea wagonjwa
- kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wasichana shuleni.